KUFUATIA madai ya wasanii wengine wengi wanaosema kuwa, msanii kujiingiza kwenye siasa ni kuishiwa, nyota wa kike wa filamu za Kibongo Chuchu Hans ameibuka na kujitetea.
Chuchu amesema, sanaa na siasa vina uhusiano
mkubwa na kwamba mtu anapojitumbukiza kwenye sanaa tu anakuwa tayari ni mwanasiasa hata kama hajatangaza nia.
“Mi nafikiri ni mawazo duni tu ya baadhi ya wenzetu kudai kuwa, msanii kuingia kwenye siasa ni kuishiwa,” alisema Chuchu Hans huku akibainisha kuwa binafsi, yeye ni mwanasiasa.
No comments:
Post a Comment