Barvetta Singletory, 37- msaidizi maalumu wa Rais na masuala ya kibunge Ikulu
Mfanyakazi wa White House (Ikulu ya Marekani) alikamatwa na kupewa likizo isiyo na malipo baada ya kutuhumiwa kunyakua bunduki ya mpenzi wake na kumfyatulia risasi wakati wa malumbano makali, polisi walisema Jumatatu.
Barvetta Singletory, 37- msaidizi maalumu wa Rais na masuala ya kibunge Ikulu – alikamatwa Ijumaa baada ya tukio hilo.
Aliripotiwa kumshambulia mpenzi wake, afisa wa polisi wa Capitol Hill, ambaye alimuona msichana mwingine kabla ya kukwapua simu zake mbili na bunduki ya 40 caliber, NBC iliripoti.
Ikulu ya Marekani maarufu kama White House
Wakati polisi huyo alipokataa kumpa Singletory passwords (nywila) za simu zake, alichukua bunduki na kumuelekezea, akisema: “Ulinifundisha namna ya kutumia hii. Usidhani sitoitumia,” kwa mujibu kibali cha kukamatwa.
Polisi walisema alimuelekezea bunduki hiyo na kufyatua mara moja.
No comments:
Post a Comment