Polisi
mkoani Kilimanjaro wakiwa wameuzuia msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na
Mgombea Urais kupitia Chadema na anaeungwa mkono na UKAWA, Edward
Lowassa katika kijiji cha Maroro, Wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro, wakati anakwenda kuhudhuria mazishi ya Kada na Mwasisi wa Chama
cha Mapinduzi CCM, mzee Peter Kisumo huko Usangi.
Viongozi wa upinzani waliokua katika msafara huo.
Msafara ukiwa umesimama
Polisi wakiwa wametanda.
Edward Lowassa akizungumza jambo.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akijaribu kuzungumza na Polisi.
Mbatia akifafanua jambo kwa Wanahabari kuhusiana na zuio hilo la Polisi.
Lowassa akizungumza kwa simu huku akiwa na Mbunge wa Moshi Mjini Mzee Philemon Ndesamburo.
Edward Lowassa akizungumza na wanacham wa vyama mbalimbali waliojitokeza kumlaki na kumsimamisha katika eneo la Boma Ng'ombe
***************
Baada
ya polisi kusisitiza kutoruhusu msafara mzima uende mazishini mgombea
huyo aliamua yeye na maofisa wengine alioambatana nao kurudi Mwanga
akisisitiza asingeweza kwenda peke yake akiwaacha watu aliambatana nao.
***************
Polisi
mjini Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais
kupitia Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria
mazishi ya kada wa CCM, Peter Kisumo.
Vyanzo
vya kuaminika toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara huo
kutokana na kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi wa
Ukawa na wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi hawakuafiki.
Taarifa
zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi lilizusha
mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende mazishini
peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee yalikotoka
jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.
No comments:
Post a Comment