Baadhi ya Wana CCM wakiwa katika moja ya mikutaano yao wakati wa kujitambulisha kwa wagombea Ubunge na Udiwani walipotembelea na kujinadi kwao hivi karibuni. Pichani ni wana CCM wa Kata ya Magomeni kama wanavyoonekana hivi karibuni (Picha na Maktba ya modewjiblog).
Na Andrew Chale, modewjiblog
Kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) zimeendelea kupamba moto kwa sehemu mbalimbali wana CCM kujitokeza kupiga kura kuchagua kiongozi wao atakaye wafaa ndani ya CCM ambaye baadae atasimamishwa kuwania kiti hicho katika uchaguzi wa hapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Wana CCM wote wenye kadi kihalali ndio wenye fursa ya kupiga kurfa hizo za maoni tayari wameanza mchakato huo mapema asubuhi zoezi linaloendelea hadi hivi sasa na baadae maatokeo yataanza kutaangazwa/ kutolewa kwa kila eneo husika na kisha kutangazwa huku yale ya Udiwani yakitarajiwa kutangazwa katika ofisi za CCM Kata na Ubunge kutangazwa Ofisi za CCM Wilaya.
Awali wagombea hao walipita kila eneo na kujinadi ndani ya wana CCM kwa lengo la kujitambulishwa na kunadi sera zao ilikupata fursa ya kuchaguliwa/kupitishwa huku tukishuhudia mambo mbalimbali kutoka kwa watangaza nia hao. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na tukio la aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai kumpiga mtu katika uchaguzi na kumsababishia maumivu makali hadi kupoteza fahamu.
Mbali na hilo la Job Ndugai, pia baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa wapo baadhi ya wagombea Ubunge na Udiwani wakishutumiwa kutoa rushwa kwa wana CCM huku wengine wakikanusha kwa hilo.
Modewjiblog ipo katika mitaa mbalimbali kuanzia asubuhi hii ikikusanyia matukio ya uchaguzi huu wa kura za maoni ndani ya CCM, na kisha tutawaletea hapa hapa moja kwa moja ilikujua nani kapenya na nani amebaki….
#Mo Blog
No comments:
Post a Comment