Saturday, July 4, 2015

MWANAUME: OA MWANAMKE ANAYEKUPENDA, SIO ULIYEMTENGENEZEA MAZINGIRA AKUPENDE..UTAJUTA MBELENI...

Habari za wakati huu, Muwazima?..
Baada ya salamu, mimi mwaka huu nimedhamiria kuwakomboa wanaume wenzangu kwenye majanga ya mapenzi, maana wengi katika wao, wanasumbuka mno! Naomba nianze kuifafanua hiyo heading hapo juu. Juzi kati hapa nilileta tofauti kati ya kupendwa na kuonyeshwa mapenzi, wengi walielewa, lakini wengine bado wanaendelea kuwang'ang'ania waonyeshaji mapenzi, but that'z none of my business! Cha msingi mimi nimewazindua.

Leo, tuje hapa, kwa mara nyingine tena! Ewe ndugu yangu, mwanaume mwenzangu, kwanini uoe mtu asiyekupenda? Mtu uliyemtengenezea mazingira akupende kwanini? Unaoaje mwanamke uliyemtongoza miezi sita? Mwaka mmoja? Miaka miwili? Mwanamke mwenye mapenzi na anayejua haswa thamani ya mapenzi hatongozwi miezi 6 au mwaka mzima banaa. Mimi hata mwezi kwanza siwezi naanzaje kukuchombeza mwezi mzima? Unataka usome nini kutoka kwangu?

Hawa wanawake wa kutongozwa muda mrefu hawajatoa majibu ni wanawake wanaokuchunguza na kukulinganisha na watongozaji wengine na wewe bado unang'ang'ania tu kutongoza.

Hapa kuna matokeo mawili muhimu sana:
1. Kuna uwezekano mkubwa akakukubalia baadae kwa moyo mmoja tu, tena kwa nia njema. Hii ni kwa sababu umemtengenezea mazingira, amekuona unafaa, na katika kipindi hicho kirefu cha kumbembeleza na kumuomba majibu kuna mengi umemtendea.

Ameyakubali, umenunua sana vocha, out sana umemtoa, umejali na kuzitambua sana baadhi (kama si zote) ya shida zake, sasa asikupende kwanini?! Na principle ni kuwa Moyo umeumbwa kumpenda anayeufanyia wema na kumchukia anayeutendea mabaya.Sasa unataka ufanye mazuri halafu moyo usikupende?! Utakupenda tu. Lakini Je, unadhani wewe ndo mfanyaji mazuri peke yako? Mazuri uyafanyayo wewe unahisi ndo yanayomtosheleza?! Be careful!

2. Kwa kipindi chote hicho unachong'ang'ana kutongoza, labda miezi 6 yako au mwaka, atakuelewa na kuusoma udhaifu wako wootee.Halafu atakukubalia! Ataishi na wewe kimjinimjini na kukufanya zoba huku akiendelea na vidume vingine kimyakimya bila wewe kushtukia! Utashtukia vipi sasa wakati ulipokuwa unabembeleza ukubaliwe ulijisahau na kuanza kujionyesha jinsi ulivyo na udhaifu wako wote! Umshtukie? Wapi.

Hivi hujui kuwa wakati wa kutongoza ndo mwanaume anaposema vingi vya ukweli kumuhusu yeye? Hata kama wewe ni mdanganyaji mzuri, jichunguze ukiwa unatongoza, unavyofunguka. Sasa unaanzaje kutongoza miezi sita? Ili ufunguke vyote kuhusu wewe na ukoo wako? Au unataka ugundue nini. Hayo 1 & 2 hapo juu yote hayapo upande wako mwanaume mwenzangu, kwahyo jiongeze baba.

Nahitimisha sasa;

Dalili kuu ya kwanza ya mwanamke wa maslahi/asiye na mapenzi ya kweli ni kutongozwa muda mrefu! Chunguza vizuri utajijibu.Yaani ukiona unabembeleza wee ujue utkubaliwa, maana wakibembelezwa sana hawakatai hao, anaweza akakukubalia kwa sababu ya kukuonea huruma tu ili uridhike, au kwa ushauri tu wa mashoga zake baada ya kuwaelezea jinsi unavyopata tabu kuwa makini sana.

Hii statement ya kizungu niliiokota sehemu, nadhani inaweza kukufungua akili kidogo:
Decision Making is easier when there is no Contradictions into your value system .
Kwahiyo ukiona decision making yake ni ngumu, ujue hapo kuna kinyume na hiyo statement hapo, Contradictions zimetawala. Angalia sana kijana mimi ushauri wangu, please.

Usijiendekeze bana, tongoza, bembeleza, onyesha nia ya dhati. Kama kweli maneno yanatoka moyoni, yataingia tu kwenye moyo wake tena kirahisi.Kama atashawishika atarespond mapema tu na kama hataki na anajitambua atakwambia "Mi nina mpenzi/occupied" usilazimishee. Utakua unamtengenezea mazingira tutarudi kulekule! Kwani wewe ukiwa na msichana ungependa atoke na msela mwingine? Sasa kwanini wewe unataka kutoka na mademu wa wenzio?

Akikwambia haiwezekani au nina mpenzi, geuka kulia na kushoto vuka barabara hamia upande wa pili huko, wapo kibao. Wanaume sisi ni wachache kuliko wanawake, sasa unaanzaje kubembeleza mtu miezi au miaka, ili? Akutangaze au?! Wengine wanabembeleza sana eti wanaogopa kuonekana wamekataliwa!


Wee ni bora ukataliwe kuliko kujifanya kidume halafu ukaanza kutengeneza mazingira upendwe usipopendwa madhara yake ni makubwa. Nimeeleza hapo juu!.Kwanza ukweli ni kuwa watoto wa mjini ndo wanaogongwa na magari, wale wa kijijini wanachukua tahadhari sana kwenye kuvuka, lazima waangalie kushoto, mara kulia ndo avuke. Sasa wewe wa mjini gani unaogopa kutoswa bana?! Ngoja nkale daku nilale, nikimaliza UE nitarudi hapa kuwapa trick jinsi ya kutokea siku ya kwanza ya kutongoza.

No comments:

Post a Comment