KUTIA alama mwilini umekuwa utamaduni kwa miongo kadhaa katika maeneo tofauti barani Afrika ili kuashiria urithi wa kikabila.
Vitendo hivi hata hivyo vinapungua lakini bado kuna watu wanaotaka
kuendeleza kilichofanya na mababu zao.Katika mji wa Ouidah kaskazini mwa
Benin, kuna tambiko inayotarajiwa kufanyika ikifuatwa na siku mbili za
sherehe.
Huneda ni mojawapo wa makabila nchini Benin inayoamini kuwa tendo la kuchanja watoto – hasa usoni- huwaunganisha na mababu zao.
Watoto hao hupewa majina mapya, wananyolewa vichwa vyao na kupelekwa
katika makazi ya watawa ambapo kuna mizimu inayowasaidia kuzungumza na
vizazi vya hapo awali.
'Utamaduni unaoenziwa'
“Hii ni sehemu ya tamaduni zetu na ni muhimu sana kwangu,” anasema
Genevieve boko, ambaye mwanawe wa kike mwenye umri wa miezi 6, Marina,
pamoja na wapwa zake Luc na Hospice wenye umri wa miaka 10 na miaka 12
wote wako tayari kuchanjwa.
Mpekuzi ilifanya mahojiano na mama huyo ambaye naye alionyesha
kushangazwa na tukio hilo na kusema hajui tatizo lililomfanya ajifungue
mtoto huyo kwa kuwa hakuwahi kusikia maumivu ya aina yoyote wakati wa
ujauzito huo hadi alipofikia hatua ya kujifungua….
Katika mahojiano hayo, mama huyo alisema kuwa huo ni uzao wake wa 6 na hajawahi hudhuria Clinic
Jivu hutumika kutia alama sehemu ambayo chanjo hiyo hufanywa na huchukua sekunde chache chanjo hiyo kufanya.
“Rafiki zangu waliniuliza iwapo ni uchungu na iwapo nililia na nikasema ‘la!’,” alisema Luc baadae. “Kabla, nilipokuwa
nikitembea mitaani pamoja na ndugu yangu mkubwa aliye na makovu, watu
hawangeamini kuwa ni ndugu yangu. Sasa nina furaha kwa kuwa
tunafanana.”Tangu mume wake alipoaga dunia, Gamba Dahoui amekuwa
akifanya chanjo zote za nyumbani-anasafisha vifaa vya kuchanjia kwa
mimea yenye dawa pamoja na tembo. Makaa pia huwekwa kwenye majeraha ili
kuyasaidia kupona.
Dahoui hutumia kisu kimoja tu kila wakati, huku akipuuza mashari rasmi
ya kutumia nyembe safi kwa kila mtu ili kuepuka hatari ya kuambukiza
magonjwa yanayoambukizwa kwa damu kama vile pepopunda na UKIMWI.Chanjo
hizi hata hivyo zimeanza kupoteza umaarufu. Idadi kubwa ya familia
inashiriki sehemu ya kwanza tu ya sherehe hizo, na kuacha kabla ya
chanjo kufanywa.Ni sawa sawa na sehemu mbalimbali ya taifa hilo ambapo
kila kabila huwa na mfumo wake wa kuchanja.
'Ni aibu kukosa alama au makovu'
“Nikiwa na makovu yangu, ninatambulika kila mahali ninapokwenda,”
anasema Fleury Yoro, anayeishi Atacora, kaskazini mwa taifa hilo. “Iwapo
ningepata nafasi ya kufanya uamuzi, singependa kuwekewa makovu namna
hii.”
Anasema kuwa alipokuwa akisoma katika jiji kubwa zaidi nchini Benin
Cotonou, alikejeliwa mara kwa mara kutokana na makovu yake. Watu kadhaa
‘‘hawangependa watu wengine wadhani kuwa walikuwa marafiki na mtu
mshenzi namna ile,” anasema.Wengine wana maoni tofauti ya kufanya uamuzi
wa kutochanja vizazi vichanga. Sinkeni Ntcha aliacha kitendo hicho
baada ya watoto wake 3 wa kwanza ‘‘kwa sababu ya UKIMWI,” anasema.
‘‘Nyembe zinapaswa kubadilishwa kila wakati lakini wakuu
walikataa.”Kwake, kama mmoja kati ya watu wa kabila la Otomari, alama
hizo “hazina maana”. Utamaduni unawezwa kuendelezwa kwa njia nyingine,
anasema, kupitia kwa lugha, densi, unyago na usanifu.Watu wengi wa
kabila la Otomari bado wanakubali kutiwa alama, wakiwemo wanawake kadhaa
wachanga ambao wakati mwingine huchanjwa kwenye migongo yao na tumboni
wanapobalekhe ili ‘‘kuonyesha ujasiri wako,” anasema Edith
(aliyeonyeshwa kwenye picha). Mifumo huwa sawa mara kwa mara na michoro
inayochorwa kwenye mijengo ya mitaani.
Wakati mwanawe Genevieve Boko, Marina (hapo chini) alipokuwa na umri wa
miezi 6 tu alipotiwa alama – watoto katika sehemu zingine nchini Benin
hufanyiwa kitendo hicho juma moja tu baada ya kuzaliwa.
Katika nchi jirani ya Nigeria, suala la haki za watu wachanga
limesababisha baadhi ya majimbo kupiga marufuku zoezi hilo kwa watoto
wote.
Hata hivyo, hii sio hatua inayowapendeza watu wote wa Benin. ‘Hatukiuki
haki za watoto, tunawaonyesha watoto walikotoka na kile watakachopitia
maishani,” anasema Telesphore Sekou Nassikou, mhariri mkuu wa kituo
kimoja cha redio mjini Natitingou iliyoko kaskazini magharibi mwa taifa
hilo.Kwake, makovu hayo hupitisha ujumbe: ‘‘Tahadhari, kuna uchungu
katika dunia hii, na utahisi uchungu katika maisha yako. Hata hivyo
uchungu huo utaisha iwapo utavumilia
No comments:
Post a Comment