Je, umewahi kuwaza kuhusu hili la mbegu za kiume kuvunwa?
Sasa imeelezwaa kwamba ni vyema mbegu za uzazi wa wanaume zikavunwa na kuhifadhiwa mara tu pale mtu anapotimiza miaka 18.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtafiti wa maswala ya uzazi nchini Uingereza Daktari Kevin Smith, amesema kuwa manii ya mwanaume huwa katika hali bora zaidi wakati wa umri huo na hivyo mbegu zinapaswa kuvunwa na kisha kutumika kupandikiza wanawake katika siku za usoni.
Daktari Smith, ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo kikuu cha Abertay kilichoko Dundee nchini Uingereza amesema kuwa baada ya utafiti wa kipindi kirefu amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ili kuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.
Dk. Smith, anasema kuwa Wizara ya Afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi ili kupunguza visa vya maradhi aliyoorodhesha.
Pamoja na maoni hayo ya Dk. Smith. Wauguzi wa masuala ya uzazi wameonekana kupinga jambo hilo na kusema kuwa njia hiyo haitakuwa suluhishi la kudumu.

Mbali na hayo, akitetea wazo lake katika jarida la madaktari la ''The
Journal of Medical Ethics, Dakta Smith amesema kuwa wale wanaotaka
kupata watoto mapema basi wafanye hivyo, lakini kwa wale ambao wamegonga
miaka 40 ni vyema watumie mbegu walizohifadhi kwa matokeo mazuri zaidi.
Takwimu zinaonesha kuwa wanaume wanaanza kupata watoto wakiwa na umri wa miaka 33 ikiwa ni ongezeko kutoka kwa miaka 31 katika miaka ya tisini, lakini mwanasayansi Sheena Lewis, aliwashauri wanaume waanze kushughulikia swala la familia mapema katika ujana wao.
''Ninataka kuwaelezea wazi kuwa umri mzuri wa kuzaa kwa wanaume na wanawake ni kati ya miaka ya 20 na 30." Alisema mwanasayansi Lewiis.

No comments:
Post a Comment