Sunday, June 28, 2015

ZIARA YA KINANA KATIKA JIMBO LA NYAMAGANA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi kutoka wilaya ya Nyamagana wanaounda makundi ya Machinga,Bodaboda, na Mama Lishe kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na makundi ya Mama Lishe ,Machinga na Boda boda katika kikao kilichofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
 Baadhi ya Mama lishe waliohudhulia kikao na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana kwenye ukumbi wa BOT mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na taarifa ya kazi za Chama.
 Daraja la zamani la Isegeng’e lililopo kata ya Mahina.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa daraja  jipya la Isegeng’e, kata ya Mahina wilaya ya Nyamagana.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa CCM Igoma.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Igoma wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Igoma na kuwaambia kuwa wachague viongozi wanaojali watu ili kusaidia kuleta maendeleo kwa haraka.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimia wakazi wa kata ya Buhongwa wakati wa ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la CCM Buhongwa.
 Wakazi wa Buhongwa wakifurahia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM wakati wa sherehe za ufunguzi wa kitega uchumi cha CCM kata ya Buhongwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Buhongwa na kuupongeza Uongozi wa kata ya Buhongwa kwa kujenga kitega uchumi hicho kushirikiana na muwekezaji wa ndani.
 Umati wa wakazi wa kata ya Buhongwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Vijana wa Nyegezi wakimpokea katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa shangwe ya kipekee.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akizungumza wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM na Vijana wa Boda boda wa Nyegezi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu Vijana wa Boda Boda wa Nyegezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Vijana wa Boda Boda wa Nyegezi ambapo aliwaambia ni vyema kuchagua viongozi watakaosaidia Vijana katika maendeleo yao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera wakati wa uzinduzi wa Shina la UVCCM Bungeni,Nyegezi wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza. (Picha zote na Adam Mzee)

RAY C FOUNDATION YASAIDIA VIJANA ZAIDI YA 70 KUACHANA MADAWA YA KULEVYA

DSC_0087
Mwanadada aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akihojiwa na wandishi wa habari wakati wa kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.
Na Andrew Chale, Modewjiblog, Bagamoyo.
***********
MWANADADA aliyewahi kung’ara katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesema moja ya sababu iliyomfanya kuanzisha taasisi yake ya  kupambana madawa ya kulevya ya Ray C Foundation, ni kutaka kuelimisha vijana na jamii nzima juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya na athari zake.
Ray C alieleza hayo wakati wa kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu maadhimisho yaliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 26 huku Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mgeni rasmi kwenye kilele hicho.
Ray C  alibainisha kuwa kwa sasa kupitia taasisi hiyo tayari ameweza kusaidia vijana mbalimbali kuachana na dawa za kulevya.
Pia kupitia taasisi yake hiyo, vijana mbalimbali wameanza kubadili tabia ikiwemo kuanza kutumia dawa za kuachana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya Methadoni.
“vijana zaidi ya 70, wameweza kubadili tabia ikiwemo kuanzishiwa matumizi ya dawa maalum za kuachana na uteja yaani dawa za Methadone.” Alibainisha Ray C.
Aidha, kwenye maadhimisho hayo Ray C aliomba wazazi kusaidia vijana wao waweze kuwapeleka kupatiwa matibabu ya kuachana na dawa za  kulevya katika vituo vilivyopo hapa nchini  ikiwemo Mwananyamala, Temeke na ama kuwasiliana na vituo vya Soba vilivyopo kote nchini.
DSC_0082
Mwanadada aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akihojiwa na wandishi wa habari wakati wa kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.
DSC_0066
Mwanadada aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki, Rehema Chalamila ‘Ray C’  akiwa na mmoja wa maafisa wa taasisi yake wakati wa  kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.

KINGUNGE ANUSA MCHEZO MCHAFU URAIS NDANI YA CCM

Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Kingunge Ngombare Mwiru.
*********
Dar es Salaam. 
Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Kingunge Ngombare Mwiru (Pichani) amesema anahisi kuna mchezo mchafu unapangwa kwenye mchakato wa kupata mgombea wa urais wa chama hicho tawala, akitaja idadi kubwa ya waliojitokeza kuwa ni ishara mbaya.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliyefanya kazi na marais wa awamu zote nne, pia, bila kumtaja jina, alitumia muda mwingi kwenye hotuba yake kujibu kauli ya makamu mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula aliyekaririwa akisema kuwa mgombea wa chama hicho hatakiwi kujinadi.
Kingunge, ambaye amejitokeza hadharani kumpigia debe Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alionyesha hofu hiyo jana wakati mbunge huyo wa Monduli alipokuwa akihitimisha kazi ya kusaka wadhamini mkoani Dar es Salaam kwenye ofisi za CCM Mkwajuni wilayani Kinondoni.
Hadi sasa, makada waliochukua fomu kuwania urais kwa tiketi ya CCM ni 41 baada ya mwanachama mmoja kuchukua fomu jana akisema atamudu kupata wadhamini kwa njia ya mtandao katika siku tano zilizosalia. Akizungumza katika mkutano wa kusaka wadhamini ulioandaliwa kwa ajili ya Lowassa wilayani Kinondoni jana, Kingunge alipingana na kauli ya Mangula kuwa mgombea wa CCM atanadiwa na chama, si kujinadi mwenyewe akisema chama hicho kinataka mgombea anayekubalika ndani na nje.
Siku tatu zilizopita, Mangula alihojiwa na kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) na kusema mgombea wa chama hicho hatakiwi kujinadi mwenyewe, kusisitiza kuwa anatakiwa kunadiwa na chama.
Lakini Kingunge aliikosoa kauli hiyo jana akisema chama hicho kimeweka utaratibu na hakuna sababu ya kuuacha na kuanza kuwahukumu wagombea kabla ya vikao na kusisitiza kuwa CCM haikuwahi kuwahukumu wagombea kabla katika chaguzi zilizopita.
“Mchakato ufuate taratibu zilizowekwa,” alisema Kingunge ambaye aliibuka Kinondoni ambako Lowassa alimalizia shughuli zake jijini Dar es Salaam.
“Nimemsikia kiongozi wetu mmoja tena juzi juzi hapa, nikamuona kwenye televisheni anasema mtu hawezi kwenda kujinadi yeye binafsi, ananadiwa na chama.
“Nikasema eh! hilo hilo. Lakini nataka nimweleze yeye na wenye fikra kama hizo kuwa kuna ngazi mbili katika utaratibu wetu; kwanza, mwanachama anayetaka kuwania ubunge, udiwani, urais lazima ajinadi ndani ya chama, ndivyo tulivyofanya miaka yote kwa mujibu wa katiba na taratibu zetu. Ndivyo wanavyofanya sasa wakina Lowassa.”
Alisema pili, wagombea wakishajinadi chama kitamteua mmoja ambaye kitamnadi na yeye ataendelea kujinadi.
“Si vizuri watu ambao tumewapa vyeo katika chama wakaanza ama wakaendelea kukitumia chama chetu kwa mambo yao binafsi. Kama wana mashaka tupo tunaojua mambo ya chama,” alisema Kingunge huku akishangiliwa na mamia ya watu.
Kingunge alisema mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa Dodoma alisema chama kinatafuta mgombea anayekubalika ndani na nje ya chama hicho ili kuweza kushindana na vyama vingine.
#Mwananchi

WACHEKI KABLA NA BAADA YA MAARUFU AY, SALAMA, AMINI NA LINAH!!! *PICHAZ*


AY & SALAMA JABIR
#ZAMANI

AY & SALAMA JABIR SASA
  
LINAH & AMIN #TBT
 
LINAH & AMIN #SASA

IDADI YA WALIOUAWA HOTELINI TUNISIA YAZIDI KUONGEZEKA

 
Waliouawa na wakitolewa eneo la ufukweni.
 
Eneo la ufukwe ambapo shambulio hilo lilitekelezwa.
 
Waliouawa, miili yao ikiwa imefunikwa.
 
Mmoja kati ya waliotekeleza shambulio hilo akipewa kipigo baada ya kukamatwa na Maofisa wa Ulinzi wa Tunisia.
 
Maofisa wa Ulinzi wakiimarisha ulinza eneo la tukio.
 
Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi akimsalimia mmoja kati ya majeruhi wa shambulio hilo.
Sousse, Tunisia
Kutokana na shambulizi la wenye silaha katika hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye Ufukwe wa Pwani ya Tunisia jana, idadi ya watu waliokufa imefikia 38 mpaka sasa huku wengine 36 wakiwa majeruhi.
Maofisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na Maofisa wa ulinzi wa nchi hiyo na kuwa waliosalia bado wanasakwa na Jeshi la Polisi.
Kundi la wapiganaji wa ISIS wamethibitisha kutekeleza shambulio hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika Mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka Bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.
Waziri Mkuu wa Tunisia, Habib Essid amesema kuwa, miongoni mwa watalii hao wengi wao walikuwa ni raia wa Uingereza, na wengine wanatoka Ujerumani, Ubelgiji na nchi nyingine.
Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli za watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni kuanza kuwamiminia risasi mpaka kusababisha mauti watalii hao.
Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunisia.
October 2013, Mlipuaji wa kujitoa mhanga, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya Maofisa wa Polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia.
CHANZO BBC NA DAILY MAIL

WASICHANA WA AINA HII NI HATARI SANA KUWA NAO KIMAPENZI

Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..

1.Demu wako wa zamani 
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakikamwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.

2.Dada wa rafiki yako kipenzi
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako.
Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

3.Wanawake wenye mambo mengi
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salamakuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote.

4.Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)
Kuwa mbali nao, labda kama unatakasalio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi.

5.Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.Wadau mademu wapo wengi sana, fanya kutafuta wengine nje ya hawa….. ni ushauri tu.

MAMIA WAJITOKEZA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR KUMUAGA MHARIRI EDSON KAMUKARA

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam jana asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki dunia juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Reginald Mengi (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilibrod Slaa kwenye uagaji wa mwili wa Edson Kamukara. Kulia ni Mbunge wa Bukoba mjini, Khamis Kagasheki.
Mmoja wa waandishi wa habari akiwa amepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo.
Wanahabari na waombolezaji wengine wakiwa wamejipanga foleni wakati wa utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea (katikati), akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Wanahabari ni huzuni na vilio.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki wakati wa kuuaga mwili wa Edson Kamukara.
Wanafamilia ya marehemu wakiwa kwenye shughuli hiyo.
Sehemu ya umati wa watu katika shughuli hiyo.
Mwakilishi wa wanafunzi waliosoma na marehemu Shule ya Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi akizungumza kabla ya kutoa rambirambi yao ya sh.500,000.
Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Paul Makonda akizungumza katika uagaji wa mwili wa marehemu ambapo alipigania waajiri wa vyombo vya habari kutoa mikataba ya ajira kwa wanahabari.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi akimfariji Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea alikuwa akifanyakazi marehemu Edson Kamukara.
Ni vilio tu kwa wanahabari.
Shughuli ya uagaji ikiendelea.
Dada ya marehemu Edson Kamukara akitoa heshima za mwisho.
#Habari za jamii.com