Naibu Waziri wa Fedha, Lameck Mwigulu Nchemba jana jina lake liliingia kwenye headlines baada ya kutangaza kujivua kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara.. hiyo ishu ilichukua nafasi kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii kuanzia siku ya jana May 24 2015, leo anayeingia kwenye headlines ni Nape Nnauye, Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM amezungumzia kuhusu ishu ya Mwigulu Nchemba alivyojitoa kwenye nafasi yake hiyo ndani ya Chama.
>> “Tumejadili mambo mengi nikaona hili moja nilitoe mengine tutaendelea kupeana”>>> Nape Nnauye.
>>> “Mwishoni mwa kikao Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara ndugu Lameck Mwigulu Nchemba ameomba kwa Halmashauri kuu ya Taifa kupumzika kwa sababu ya nia yake ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wa nafasi ya Urais”>>> Nape Nnauye.
>>> “Ametumia busara na wajumbe wameridhika, wamepongeza busara yake”>>>
>>> “Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa akamteua Rajabu Luhavi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ikampitisha kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Tanzania bara.. amekuwa msaidizi wa Rais Ikulu mambo ya siasa sasa anahamia kwenye chama”>> Nape Nnauye.
Kama unataka kuisikiliza sauti ya Nape Nnauye unaweza kuplay hapa umsikie akimzungumzia Mwigulu Nchemba.
No comments:
Post a Comment