Ugonjwa wa macho mekundu huyafanya macho yakawa mekundu, yakauma na yakavimba
Ugonjwa wa macho mekundu ambao uliwakumba wanafunzi wengi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2013 umerejea tena kwa baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Taarifa News ilifanya uchunguzi na kugundua kuwa maradhi hayo yamerudi tena na kuwaanza watu kwa hatua za mwanzoni.
Gonjwa hilo ambalo hujulikana kama “Red Eyes” hushambulia macho na kuyafanya yavimbe, yawe mekundu na hivyo kuwalazimu waathiriwa kuvaa miwani kupingana na mwanga wa jua.
Muonekano wa macho kwa mgojwa wa macho mekundu
Jicho ni moja ya kiungo muhimu katika mwili wa binadamu, ugonjwa wa macho mekundu, maarufu kama ‘Red Eyes’ ni moja ya magonjwa ya muda mrefu na imekuwa ni hali ya kawaida ya kila mwaka wakazi wa maeneo mbalimbali.
Mwaka uliopita maeneo ya jirani na vilipo vyuo hivyo wananchi wanakumbwa na ugonjwa huo, huku wagonjwa mbalimbali wakiripotiwa kuugua ugonjwa huo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).
Kutokana na maradhi hayo Wizara ya Afya ilitoa tangazo hili kwa jumuiya ya wanachuo;
Tangazo lilitolewa na Wizara ya Afya mwaka uliopita kufuatia kuibuka kwa maradhi hayo kwa wanachuo
Ugonjwa wa ‘Red Eyes’
Ugonjwa wa macho mekundu kwa kawaida unasababishwa na kitu kinachoitwa tabaka la juu ya jicho hali ambayo inatakiwa ilifanye jicho kuwa jeupe na linapobadilika na kuwa jekundu hapo ndipo binadamu anapotakiwa kujua kuwa tabaka jeupe linaleta chakula na hewa kwa ujumla wake. Pia vipo vimishipa kwenye macho ambavyo vinapovimba husababisha ugonjwa wa Red Eyes.
Hadi sasa chanzo halisi cha ugonjwa huo hakijajulikana kuwa unatokana na nini lakini tafiti zinaonyesha kuwa vipo viashilia vinavyoonyesha kuwa ugonjwa huo unatokana na kuwepo kwa michirizi inayokatiza kwenye jicho ambayo huathirika mfumo wa damu.
Sababu ya jicho kuvimba inatokana na vumbi, mzio/aleji na inaweza kuwa moshi, unywaji wa pombe, kuchelewa kulala na mwingine anaweza kukumbana na hali ya mishipa kujikunja hali inayopelekea mishipa kushindwa kusambaza damu kama kawaida.
Daktari Erick Matimbwi, mtaalamu wa tiba mbadala jijini Dar es Salaam, anasema sababu nyingine ya ugonjwa huo ni kuwa na ugonjwa wa Shinikizo la damu la juu na ukosefu wa vitamin A. B3 au B6 na kwamba idadi kubwa ya watu wanaweza kuambukizwa ugonjwa huo kwa wakati mmoja katika baadhi ya nchi za Afrika.
“Utumiaji wa vitamin A, B, B6 na nyingine chachu zitokanazo na vitamin za mboga za majani, matunda kwa wingi vinasaidia kuweka kinga ya kuugua ugonjwa huo pamoja na kula maharage kwa wingi kwani inasababisha vitamini B”.
Moja ya sababu inayotajwa kusababisha hai hiyo ni neon la kitaalamu lijulikanalo kamachavua katika anga hewa licha ya asili ya macho kuwa na uzio wa kuzuia kitu isichopata na acho kukizuia ili kisiingie ndani.
Aidha, imeelezwa kuwa ugonjwa huo unasababishwa na aina mbalimbali za bacteria. Watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea kwa kawaida mamcho yaop huwa mekundu kuliko vijana.
Tafiti zinaonyesha kuwa macho ya mwanadamu hayatakiwi yazidi kuwa mekundu na watu waliochini ya umri huo wanatakiwa kuwa makini wanapoona macho kuwa mekundu wazingatie kwende kwa madaktari kujua chanzo na tiba.
Mgonjwa anapohitaji tiba anatakiwa kutumia njia ya kumuona mtabibu haraka iwezekanavyo ili kujua kama jicho lina bacteria au limeathiriwa na mwanga mkali ambao pia unasababisha ugonjwa wa mamcho kuvimba na kwamba uvaaji wa miwani meusi inaweza kusababisha mikunjo ya mishipa ya damu.
#FikraPevu
No comments:
Post a Comment