WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ametoboa siri sababu za Rais Jakaya Kikwete kumhamisha Dk. Harrison Mwakyembe (pichani) katika Wizara ya Uchukuzi kwenda Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Akizungumza juzi na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kyela, alisema Rais Kikwete alimhamisha Dk. Mwakyembe katika Wizara ya Uchukuzi kwa sababu anaifahamu vyema Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuwa alishawahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Masharika na pia mwanasheria.
“Dk. Mwakyembe amehamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutokana na kuwa anaielewa vizuri na pia ni mwanasheria aliyebobea hivyo Rais Kikwete aliona atakuwa msaada mkubwa katika kuisaidia nchi,” alisema.
Hatua ya Waziri Mkuu Pinda kutoa ufafanuzi huo kulifuatia kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi walihoji kwanini Dk. Mwakyembe amehamishwa Wizara ya Uchukuzi ambayo aliimudu vyema kwa kudhibiti vitendo vya wizi hususani katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na upitishwaji wa dawa za kulevya katika viwanja vya ndege.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), walifanya mkutano Jijini Nairobi na Rais Kikwete alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa EAC huku Waziri Mwakyembe akichaguliwa
No comments:
Post a Comment