Fredrick Bundala ambae amekuja na kitabu kinachozungumzia maisha ya Mtemi Mirambo wa Tabora, akizungumzia kitabu hicho amesema ni idea iliyozoeleka nchi za nje na baada ya kupitia mitandao akagundua Audio box kwenye soko ni kitu kikubwa sana na anapenda sana kusimulia matukio kama alivyowahi kufanya katika documentary kuhusu Mv Bukoba akaona anauweza kufanya kitu kwa kusimulia na watu wakakipenda akatengezena kitabu katika mfumo wa sauiti (Audio Box) kinachoitwa Mtemi Mirambo (Sultani Mkuu wa Afrika)
Baadhi ya wasanii wameonekana kuhamia kwenye siasa kama Mr Two, Prof. Jay, Afande Sele na wengine msanii Juma Nature amesema alikuwa amepanga kufanya hivyo na watu walimfata ila mwa mkwa huu ameona asigombee, kama angegombea Ubunge Temeke angepita ila kwa sasa amewaachia wasanii wenzake, ikitokea akawa Mbunge jambo la kwanza kufanya kwa wanachi wake ni barabara ya Mbagala, Hospitali pamoja na Soko na ataingia chama chochote atakachoona kinamsingi mzuri.
Wasanii wengi wa Bongo Flava wameendelea kujiingiza kwenye biashara, 255 leo imepiga story na msanii Ruby ambae amesema anapenda kuwa designe, anatarajia kuja na kitu kinachoitwa ‘Kilemba cha Ruby’ ambayo inahusuana na mambo ya fashion, idea ambayo imekuja kutokana na kupenda kudesigne vilemba toka akiwa mdogo ingawa kipaji chake kikubwa ni kuimba.
No comments:
Post a Comment