Sunday, March 1, 2015

MFAHAMU IRENE SANGA; MCHEZA SINEMA, MUIGIZAJI, MWANDISHI NA MWANAMUZIKI


MSANII mwenye kariba ya kimataifa Irene Sanga anasema bado hajaachana na sanaa na kwamba zipo kazi nyingi amezifanya na nyingine zipo katika hatua mbalimbali na kwamba mashabiki wake watarajie kazi njema na zenye maana katika maisha yao. Beda Msimbe  amefanikiwa kuzungumza anaye Msanii huyu ambaye kwa sasa anatamba na mchezo wa jukwaani wa Africa Kills Her Sun ambao tayari umeoneshwa nchini marekani na Uganda. Fuatilia mahojiano haya:


SWALI:

 Ghafla haupo katika ulimwengu wa muziki wala sinema nini kimetokea? au majukumu ya uzazi yamezidi?
JIBU:
Hapana watoto wameshakuwa wakubwa ,mimi nafanya sanaa kama kawaida. Siku hizi naandika filamu. Nimeandika, Mikono salama ameprojuzi JB, nimeandika Kutakapo Kucha ameprojuzi Malalo na kuchezwa na Kitime; nimeandika Nyuma ya Pazia anaprojuzi Mtitu na ninafilamu inaitwa Mjomba ndio naendelea kuiandika pamoja na Nguvu ya Msamaha ipo katika drafti ya pili. Pia nina projekti ya Afrika inaua mwangaza wake ambayo tutaanza kuifanyia mazoezi kw amaonesho ya hapa nyumbani .Mara ya kwanza tulionesha Uganda Novemba mwaka jana
Aidha naandika  telebision series za Ubongo kids na kila kilenga. Pia nimeandika skripti za Babu Mbuyu za watoto bado zipo njiani kutoka chini ya kampuni ya Tanarea.

SWALI:
 Kumbe mwenzangu unahangaika katika sanaa mimi nadhani umetulia.
JIBU:
kweli kaka nipo sana na naandikaa vitu vingi mpaka muziki. kama unavyojua muziki upo damuni.

SWALI:
Naam naelewa mashairi yako huwa yanakuwa na moto mkali hasa katika jamii. Lakini kimya kirefu.
JIBU:
Si kirefu hivyoo.Ninamiziki miwili ipo Irie Production bado sijaimaliza ,mmoja unaitwa Enjoy mwingine unaitwa Africa Bara langu.Kiufupi bado nafanya sanaaaaaa tena sanaaaaa.

SWALI
Mengi tumeyaona lakini sikuwa najua kwamba wewe umo namna hii ndio maana nikauliza. Kuna vitu watu wanavifanya halafu wanapozungumza hawasemi kuhusu wamepata wapi vitu hivyo ili watu wajue kwamba katika sanaa mtu kutengeneza chakula kilichoandaliwa na mwingine. Haya reponse (Muitikio) ya filamu ulizoandika ( Je ni simulizi au andiko lenyewe ) ipi imeleta heshima sana mjini .Na hapo hapo nikuulize kwenye muziki tutarajie kama Mjomba au safari hii mapenzi hewani?
JIBU: 
Mvuto uko katika Mikono salama.Watu wengi walinipigia simu na kusema wameipenda. Kutakapokucha pia, lakini unajua sisi waandishi huwa hatujulikani sana,watanzania hawana utamaduni wa kusoma washiriki ,filamu ikiisha tu televisheni huzimwa na wasanii wakisifiwa hawana utamaduni wa kumsifia mwandishi nadhani ni Tanzania tu ambayo ipo nyuma kwa vitu kama hivyo,watu hawapendi kumpa credit, mtu sijui ilitokea wapi hata sijui siku zote anayepika hasifiwi ila aliyenenepa baada ya kula (anacheka).Kitu kingine ni Nyuma ya pazia ninadhani itakuwa nzuri zaidi kwa sababu napenda sana kuzungumzia habari za ukweli na zinazoendelea nchini kwetu,hiyo inahusu rushwa na uadilifu kazini

SWALI:
Naam kwahiyo mwaka huu ni mwaka wetu.Haya kampuni yako inaendeleaje?
JIBU:
Namshukuru Mungu inaendelea vyema ,japo changamoto ni nyingi,kufanya kazi bila meneja ni ngumu sanaaaa

SWALI:
Hata mimi naamini hivyo lakini kwanini humtafuti meneja?
JIBU
Sijui nianzie wapi kila mara na wish (natamani) ningekuwa naye kwa sababu kazi zote hizo nilizo kwambia hakuna hata moja nilioitafutia wateja bali watu wananitafuta na ninajisikia vibaya kukaa na idea ( mawazo)  huku  sina wa kusaidia kuzipush (kufikia walengwa) ,unajikuta umekaa tu huna cha kufanya wakati nilitakiwa kuwa busy(anacheka).

SWALI
Lazima kuna kasoro. Ninavyokujua wewe ungelikuwa na nafasi kubwa ya kumpata mtu wa kufanya naye kazi au watu wa hapa wamejawa na Longolongo ?
JIBU
Kaka Msimbe  ukipata meneja niambie nikae naye tuweke miradi hadharani,namiss sana sanaa ya jukwaani nataka kuifanyia mkakati sana

SWALI:
Je kama leo mtu angelikuuliza una miaka mingapi katika sanaa na nini umekiona Tanzania ungelisema vipi?Yaani kama kioo msanii wa tanzania anakosa kitu gani 
JIBU
Nina mika 15 katika sanaa. Ninavyoona mimi sanaa ya Tanzania imeingiwa na dosari ya kibiashara kuliko ubora. Kila mtu ni msanii,kila mtu anasaka pesa ,ukisimamia ubora inakula kwako.Sanaa mbovu zimejaa mtaani huku zikinunua airtime ili ziwe maarufu hasa upande wa muziki,upande wa filamu bila skendo hujawa msanii,utandawazi uhuru wa vyombo vya habarii umeifikisha sanaa hapa,tofauti na wenzetu nchi jirani mfano Kenya na Uganda pamoja na utandawazi sanaa yao inaubora sana.

SWALI:
ulizungumzia mchezo wa Afrika inaua Mwangaza wake, je hauna mpango  hasa wa kuonesha kwa watanzania katika matamasha makubwa ya sanaa?
JIBU: 
Niliongea na Dk Martin Mhando wa tamasha la nchi za Majahazi nahisi naweza kuperfome Africa kills her sun ZIFF bado tunaangalia jinsi ya kufanya.

SWALI:
Hii naipenda zaidi ya kuonesha ZIFF, kuna haja kubwa ya sisi kuona kazi za wazawa wa nchi hii kwani wana mengi wanayasema.sasa nikuulize kuhusu msimamizi meneja anatakiwa awe na sifa zipi au meneja anatakiwa aweje, sifa zipi na yukoje. 
JIBU:
Meneja anatakiwa auze mawazo kwa wadau mabalimbali wa sanaa,mfano tukifanya mazoezi ya mchezo ajue watazamaji watatoka wapi na kuwasaka na kutangaza kwa nguvu zote:kuwasiliana wa wafanya biashara ili waweze kuwekeza katika sanaa yetu na kadhalika. Tunafasi ndogo sana imaana tunahitaji mameneja ili wapigekelele watu waje waone ukweli ni kwamba hakuna sanaa nzuri kama ya jukwaani hasa ikuchanganywa na muziki, ngoma na ucheshi .

SWALI:
Swali hili ni la kizushi .Ulizaliwa wapi, ulisoma wapi, ulijifunza sanaa wapi, Nani role model, na kubwa zaidi mashabiki wako wategemee nini?
JIBU

Nimezaliwa hapahapa Dar, nimesoma Iringa girls na Ruvu ,nimesoma sanaa Chuo cha Bagamoyo na warsha katika nchi mbalimbali. Nampenda sana Kalola Kinashe,wanaonikubali waendelee kunikubali bado nakaza buti katika sanaa sijakata tamaa.

SWALI 
bnado hujasema miaka yako?

JIBU
kaka beda nawe! Wanawake hatutaji miaka ya kuzaliwa ila kwetu Makete ,Mwenge ndio hasa nilizaliwa Ocean road hospital .
mwisho

No comments:

Post a Comment