MAHAKAMA ya juu nchini Misri imeamuru kurudiwa kwa kesi ya waandishi watatu wa Al- Jazeera waliohukumiwa kwa madai ya kuhusika na kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.
Waandishi hao wa habari wataendelea kubakia jela Watatu hadi kesi yao itakaposikizwa tena.
Hata hivyo Hakuna tarehe ambayo imetengwa rasmi lakini mawakili wa waandishi hao wa habari wanasema kuwa kesi yao itatajwa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.
Waandishi hao ambao walikamatwa disemba mwaka 2013 ni pamoja na raia wa Australia Peter Greste, Mohamed Fahmy wa Canada na Baher Mohamed wa Misri.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.
No comments:
Post a Comment