Thursday, January 1, 2015

MAKACHERO KUTOKA DAR WATUA MWANZA KUMSAKA YULE MTOTO ALBINO ALIYETEKWA JUZI *PICHA*

Mwanza.
Timu ya makachero wa polisi kutoka Dar es Saalm imewasili mkoani hapa juzi kuongeza nguvu ya kumsaka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Pendo Shilinde (4) ambaye anasadikiwa alitekwa  akiwa nyumbani kwao juzi.Tukio hilo lilitokea kwenye Kijiji cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba wilayani Kwimba saa 4:00 usiku, wakati mtoto huyo alipochukuliwa na watu wasiojulikana ambao walivunja mlango wa nyumba yao kwa kutumia jiwe kubwa, maarufu kwa jina la la “fatuma” na baadaye kutokomea naye.Polisi wametangaza dau la Sh3 milioni kwa mtu atakayesaidia kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watu waliohusika kumteka mtoto huyo.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilidai kuwa tayari watu sita wametiwa mbaroni wakihusishwa na utekaji huo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alisema ataiongoza timu hiyo inayowashirikisha pia makachero wa mkoani hapa.
Akitoa taarifa za kutekwa kwa mtoto huyo, Mlowola alisema mpaka sasa bado hawajafanikiwa kumpata licha ya kuendelea na mahojiano na watu wanne wanaowashikilia, akiwamo baba mzazi, Emmanuel Shilinde.
“Hatujafanikiwa kumpata mtoto huyu, lakini tumeomba timu ya makachero wa polisi kutoka Dar es Salaam iliyokuja kuongeza nguvu za kumtafuta na tayari wamewasili na kazi inaanza mara moja. Tutahakikisha wote waliohusika wanakamatwa,” alisema Mlowola.

No comments:

Post a Comment