Thursday, January 1, 2015

KENYATTA AAHIDI KUPAMBANA NA MAGAIDI 2015

Rais Uhuru Kenyatta.
*******
RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya ameahidi kuwa serikali yake itapambana na ugaidi na ufisadi mwaka huu wa mwaka 2015.
Rais Kenyata ameyasema hayo katika hotuba yake ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015.
Kiongozi huyo wa Kenya amesisitiza kuwa demokrasioa haiwezi kutumiwa kama chanzo cha kuchangia kuwepo kwa utovu wa usalama nchini humo na kuongeza kuwa mwaka 2015 atahakikisha kuwa raia wote wa Kenya wanakuwa salama.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwishoni mwa mwaka 2014 nchini humo umebaini kuwa raia wengi wa Kenya wanahisi kuwa bado watakabiliwa na tatizo la usalama na gharama za maisha kupanda.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.

No comments:

Post a Comment