UTAFITI uliofanyika katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka umegundua
kuwa hali ya kuwa na furaha miongoni mwa watu mbalimbali duniani kwa
jumla imeongezeka katika kipindi cha mwaka mmoja .
Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika kwenye nchi 65 ambao ulihusisha
watu wapata 64,000 furaha itokanayo na sababu mbalimbali imeongezeka
tofauti na hali ilivyokuwa mwanzoni mwa mwaka.
Utafiti huu umeoneysha kuwa angalau asilimia 70% ya watu katika
mataifa ambayo yamehusika kwenye utafiti huu wameridhika na hali ya
maisha yao jambo ambalo linaongeza furaha .
Taifa la Fiji ambalo liko kwenye bara la Oceani kusini mashariki mwa
dunia limeonekana kuwa taifa linaloongoza kwa furaha kutokana na
asilimia 93% ya raia wanaoishi kwenye taifa hilo kuridhika na maisha yao
Taifa la Fiji limetajwa kuwa taifa linaloongoza kwa furaha kwa mwaka 2014.
Kinyume na Fiji taifa la Iraq limeonekana kuwa taifa linaloongoza kwa
majonzi na furaha duni baada ya majibu ya utafiti kuonyesha kuwa taifa
hilo lina asilimia 31% pekee ya watu wanaoridhishwa na maisha yao .
Katika hali isiyiokuwa ya kawaida bara la Afrika limetajwa kwenye
utafiit huo kuwa bara linaloongoza kwa furaha ambapo asilimia 83 % ya
wakazi wa bara hilo wamekiri kufurahishwa na maisha kwa jumla .
Eneo la ukanda wa magharibi mwa bara la ulaya limeonekana kuwa eneo
ambalo watu wake hawana furaha kuliko maeneo yote kutokana na kuwa na
asilimia 11% pekee ya watu ambao wamekiri kuwa na furaha maishani mwao.
Iraq imeonekana kuwa nchi yenye furaha kwa kiwango cha chini kuliko yote duniani.
Katika utafiti huo asilimia 65% ya watu ulimwenguni kote walikuwa na
maoni kuwa mwaka 2015 utakuwa mwaka mzuri kuliko mwaka 2014 baada ya
robo tatu ya wakazi wa bara la Afrika na asilimia 26% ya wakazi wa
magharibi mwa bara la ulaya wakiwa na uhakika juu ya kupata aina Fulani
ya maendeleo katika mwaka ujao.
Utafiti huo pia umeitaja Nigeria kuwa nchi yenye hisia chanya kuliko
mataifa yote huku Lebanon likiwa taifa linaloongoza kwa kuwa na hisia
hasi kuliko yote.
No comments:
Post a Comment