VURUGU zimeibuka baina ya mafundi gereji katika eneo la Tegeta magereji ambapo polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi muda mfupi baada ya kukatiza mazungumzo kati ya mafundi hao na katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk. Wilbroad Slaa kuhusu mgogoro baina yao na mwekezaji.
Dk. Wilbroad Slaa.
Dalili za vurugu hizo zilianza kujionyesha mara baada ya askari aliyemfuata Dk. Slaa jukwaani alipokuwa akizungumza na mafundi hao pamoja na viongozi wa mitaa ya wazo, basihaya, madale, mivumoni na kisanga inayowakiliswa kwa mchanganyiko wa vyama vyote akieleza kuagizwa na Rpc Kiondoni kutotambua mkutano huo na hali ilikuwa hivi.
Hata hivyo Dk. Slaa pamoja na kuwataka utulivu aliwataka viongozi wao kufika makao makuu ya Chadema mapema wiki inayoanza na tayari kulikabidhi suala hilo kwa kurugenzi ya sheria ya chama hicho kwa hatua zaidi.
Mafundi hao ambao kwa hali isiyo tarajiwa walionyesha viongozi wa mitaa inayoongozwa na CCM pamoja na makamanda wao walipaza sauti zao wakieleza umuhimu wa kuondoa tofauti za kiitikadi katika kutetea haki za msingi kwa wanyonge.
No comments:
Post a Comment