Wananchi wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani Ludewa wakimzawadia zawadi ya mkungu wa ndizi mbunge wao Deo Filikunjombe baada ya kuwasaidia msaada wa vifaa vya maji vyenye thamani ya Tsh milioni 14.5
Na MatukiodaimaBlog
WANANCHI wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kuondokana na kero ya maji safi na salama baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kuwatimizia ahadi yake ya vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14. 5 kwa ajili ya kuvuta na kusambaza maji safi na salama ya bomba katika kitongoji hicho .
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wengine wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa hivyo jana Bi Belinada Mwenda alisema kuwa awali wananchi wapatoa zaidi ya 600 wa kitongoji hicho ambacho kimeanzishwa na jamii ya wachimbaji wa madini ya dhahabu ,walikuwa wakitumia maji machafu yanayotumika kuoshea madini na kunyweshea mifuko .
Hivyo alisema kuwa msaada huo wa maji safi na salama utasaidia kuwaepusha na magonjwa na milipuko kama kuhara na mengine ambayo walikuwa wakiyapata kutokana na matumizi ya maji yasiyo salama kwa afya ya binadamu kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka 10 sasa toka kitongoji hicho kilipoanzishwa mwaka 1992.
" Hakika tunakushukuru sana mbunge wetu kwa kutusaidia msaada wa vifaa hivi kwa ajili ya maji .....toka mwaka 1992 hadi leo tumekuwa tukiteseka kwa magonjwa mbali mbali na hata baadhi yetu kupoteza maisha kutokana na matumizi ya maji machafu ambayo tulikuwa tukitumia maji ambacho kimsingi yalikuwa ni mabaki ya maji yanayobaki katika kunyweshea mifugo na kuoshea madini"
Bi Mwenda alisema wananchi hao mbali ya kero kubwa ya maji ambayo walikuwa wakiipata ila bado walionyesha uaminifu kwa mbunge wao kwa kuendelea kubaki ndani ya CCM hadi sasa wanapotimiziwa ahadi yao hiyo kwa kitongoji hicho kuwa ni moja kati ya vitongoji vyenye msimamo na mbunge wao kwa kutoviunga mkono vyama vya upinzani .
" Kwa shida tuliyokuwa tukiipata kama maeneo mengine leo wote tungekuwa tumejiunga na upinzani ila tuliamini chama pekee ambacho kinaweza kutusaidia na CCM na ndio sababu hatukuona sababu ya kujiunga na vyama vya upinzani .....mheshimiwa mbunge wetu tunakuhakikishia kuwa kitongoji hiki hakuna hata mwananchi mmoja ambae ni upinzani na wala hatuna mpango wa kuhangaika na vyama sisi tutabanana hapa hapa CCM"
Akizungumza na wananchi hao mbunge Bw Filikunjombe pamoja na kuwapongeza kwa kutojiunga na vyama vya upinzani bado alisema kuwa ameguswa kutimiza ahadi yake kwa wakati kutokana na mateso makubwa ambayo wananchi hao walikuwa wakiyapata kwa kukosa huduma ya maji safi na salama .
Kwani alisema kuwa lengo la serikali ya CCM iliyopo madakarani chini ya Rais Dr Jakaya Kikwete ni kuona watanzania wanaendelea kuboreshewa mazingira ya maisha yao na hata kupunguza baadhi ya kero zinazoweza kupunguzw kwa wakati uliopo na ndio sababu ya yeye kama mbunge pia kuendelea kukimbiza kasi ya maendeleo ya jimbo hilo la Ludewa na kamwe hatakubali kuona wananchi wake wakiendelea kuteseka.
"Ndungu zangu wananchi wa kitongoji hiki cha Dodoma katika kijiji hiki cha Amani nimewapenda sana na ninyi wenyewe mnatambua kuwa mimi mbunge wenu nawapenda ..... hivyo msaada huo leo ni utekelezaji wa ahadi yangu niliyoitoka miezi michache iliyopita nikiwa kama mbunge wenu japo siku nilipotoa ahadi hii baadhi yenu hamkuweza kuamini kama leo ingetekelezwa ...nawaombeni sasa tunzeni vema vifaa hivi na kutunza zaidi mazingira ili kufanya chanzo cha maji kuendelea kuwa hai zaidi "
Mbunge Filikunjombe alivitaja vifaa ambavyo amevitoa ni pamoja na bomba za maji ambazo zitasambazwa katika kitongoji chote kutoka kwenye chanzo cha maji zaidi ya kilometa 20 hadi kwenye kitongoji hicho .
Kuhusu wafugaji wanaochungia mifugo katika chanzo cha maji mbunge huyo aliwataka wananchi na viongozi hao kuweka sheria ya kulinda chanzo hicho cha maji vinginevyo hakutakuwa na maana ya kuwa na bomba za maji safi ambazo zitaingiliwa na mifugo.
|
No comments:
Post a Comment