Wednesday, December 31, 2014

KESI YA MKE WA GBAGBO, YASIKILIZWA TENA *PICHAZ*

Simone Gbagbo.
****
KESI ya mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Simone Gbagbo, ambaye anatuhumiwa " kuhatarisha usalama wa taifa", imesikilizwa kwa mara nyingine tena Desemba 29 mwaka 2014.
Kesi hiyo imesikilizwa kufuatia malalamiko ya ndugu wa waliouawa katika machafuko yaliyotokea katika miaka ya 2010 na 2011 nchini Ivory Coast, ambao wamekuwa wakiomba kutendewa haki.
Simone Gbagbo.
Simone Gbagbo, mwenye umri wa miaka 65, akijulikana kwa jina la "mwanamke mwenye nguvu" alishitakiwa pamoja na viongozi wengine 82 waliokuwa wakishikilia nyadhifa mbalimbali katika utawala wa Laurent Gbagbo.
Laurent Gbagbo
Kesi hii imesikilizwa Desemba 29 kwa mara ya pili baada ya  ya mara ya kwanza kusikilizwa siku ya Ijumaa desemba 26 kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa. 
Hata hivyo kesi hiyo ilianza kusikilizwa katika mji mkuu wa Abidjan wakati serikali ya rais Alassane Ouattara ikikataa kumuhamisha Simone Gbagbo kwenda Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu  (ICC), ambayo inamtuhumu kuhusika na makosa ya " uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Washitakiwa watapaswa kujibu mashtaka ya uhalifu uliotekelezwa kati ya mwaka 2010 na 2011, wakati wa machafuko yaliotokea baada ya uchaguzi, machafuko ambayo yalisababisha vifo vya watu 3,000 kwa pande zote husika.

No comments:

Post a Comment