JESHI la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limekamata magogo ya miti yanayodaiwa kuvunwa kwenye hifadhi ya pori la serikali la Kigosi lililopo mpakani mwa wilaya ya Kahama.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema magogo hayo yamekamatwa jana na askali wa kituo kidogo cha Bulungwa yakiwa yanasafirishwa kwenda mjini Kahama.
Kamugusha amesema magogo hayo yalikuwa kwenye gari namba T731 AHT mali ya SUNVIC EXPRESS LTD ya jijini Arusha ambapo baada ya kukamatwa vibali vyake vilikuwa na utata.
Amesema vibali hivyo vimetolewa na halmashauri ya ushetu ambavyo vimeonyesha vimetolewa jumamosi December 27 siku ambayo siyo ya kazi na jumapili yake December 28 mwaka huu yalisafirishwa
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU BI ISABELA CHILUMBA.
Kufuatia hali hiyo Kamugisha amesema polisi wanafanya uchunguzi wa vibali hivyo ikiwa ni pamoja na thamani yake iliyolipwa Halmashauri shilingi 250,000/= kwa magogo 80 ya miti ya mkurungu na kama itabainika waligushi hatua zitachukuliwa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya ushetu Isabela Chilumba amesema hali ya kugushi vibali hivyo itabainika mara baada ya polisi kumaliza uchunguzi wake ingawa tukio zima linawahusisha viongozi waandamizi wa serikali wilayani Kahama kusafirisha magogo hayo.
No comments:
Post a Comment