CHEKA NA HII: BARUA KWA MCHUNGAJI
MCHUNGAJI NIRUDISHIE HELA ZANGU MI SIKUBALI
"Chonde chonde mi staki ugomvi wala nini nadai haki yangu tu.
Unakumbuka Januari 2014 nilianza kuja kituoni kwako baada kusikia habari
zako kuwa unafanya miujiza mikubwa.
Nilipokuja kwako nikakueleza
matatizo yangu ukanambia nihakikishe ninapanda mbegu kwa kutoa michango
mbalimbali ya kituo kufikia mwisho wa mwaka ntakuwa na mke, gari na
nyumba nzuri.
Mkuu tarehe 31 ndio hiyo mi niko palepale sina mke wala
mchumba, sina gari wala baiskeli na mama mwenye nyumba kanipa wiki mbili
nisipolipa deni hata pakulala ntakuwa sina, nimeshachangia karibu
milioni, nirudishie kuna mahala pengine nataka kuwekeza. Muumini wako."
No comments:
Post a Comment