Monday, December 22, 2014

BREAKING NEWS:: WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAKAZI, ANNA TIBAIJUKA AMETENGULIWA RASMI NAFASI YAKE YA UWAZIRI, PROF MUHONGO AWEKWA KIPORO

001

Mh.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia.
Wazee wa Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete amemaliza hutuba yake na Wazee wa Jiji la Dar es salaam na Kumalizia kwa Kumuwajibisha waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka kwa kutengua wadhifa wake wa UWAZIRI.

Rais Kikwete:"Waziri wa ardhi Tibaijuka kupokea pesa za Escrow , tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine."

Rais Kikwete:"Waziri Muhongo huyu tumwemweka kiporo,Waziri wa nishati na madini tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya maadili pia wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki.
Nitafanya maamuzi siku hizi mbili tatu."

No comments:

Post a Comment