SHIRIKA moja la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria limesema wapiganaji wa jihadi takriban 100 kutoka kundi la wanamgambo wa IS, wameuwawa katika siku tatu ya mapigano ya kuudhibiti mji wa kimkakati wa Kobane nchini Syria.
Shirika hilo lililo na makao yake makuu nchini Uingereza, limesema mauaji hayo yameongeza idadi ya mauaji ya wanamgambo wa IS kufuatia vita vya ardhini, kufikia 576 tangu kuanza kwa mapigano tarehe 16 Septemba.
Shirika hilo limesema wanachama wa IS walikuwa wametokea mkoani Aleppo na Raqa kushiriki vita vya kuudhibiti mji wa Kobane unaolindwa na wapiganaji wa kikosi cha cha ulinzi wa Wakurdi (YPG).
Kwa upande mwengine kikosi hicho kimetangaza kuuwawa kwa wapiganaji wake 15 katika mapigano yaliotokea Kobane jana Ijumaa huku wapiganaji wengine wa jihadi 11 waki uwawa mjini humo na pia mkoani Raqa.
No comments:
Post a Comment