Sunday, November 2, 2014

SERIKALI YAKEMEA USHIRIKINA NCHINI, WILAYA YA RUNGWE YASHIKA NAFASI YA PILI KUTOKANA NA VIFO VYA USHIRIKINA

Vifaa vinavyodaiwa kuwa ni vya kishirikina,

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Moses Mashaka amekemea tabia ya wananchi wa wilaya hiyo kukumbatia imani za kishirikina na kusababisha kushika nafasi ya pili ngazi ya mkoa. 

Alisema kuanzia Aprili hadi Septemba mwaka huu, wilaya hiyo ilishika nafasi pili kwa vifo vitokanavyo na ushirikina na kwamba hata maendeleo yamedumaa.
Alisema hayo juzi katika kikao cha Madiwani wa Halmashauri ya Busokelo, akimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo. 
“Katika kata karibu zote kwenye wilaya hii wapo watu wanaohangaika kwa imani za ushirikina na kushindwa kufanya kazi za maendeleo’’ alisema. 

Alisema mambo ya ushirikina ni imani potofu ambazo zinadumaza maendeleo na kwamba hivi karibuni katika Kata ya Lwangwa watu wawili waliuawa kwa kuhusishwa na mambo ya ushirikina. 
Alisema kupitia vikao vya madiwani vinavyofanyika ni nyema madiwani hao wakapeana kazi ya kupeleka elimu hiyo kwa wananchi ili kupunguza wimbi la vifo vinavyotokana na mabao ya ushirikina. 

Alisema kuanzia Aprili hadi Septemba mwaka huu wilaya ya Rungwe imekuwa ya pili kwa vifo vitokanavyo na ushirikina na kwamba hali ambayo ni hatari. 
Kuhusu agizo la Rais Jakaya Kikwete katika ujenzi wa maabara, alisema mpaka sasa shule nyingi bado hazijajenga maabara. 

Aliwasihi madiwani kuhimiza ujenzi wa maabara hizo ikiwa ni hatua ya wananchi kutii amri ya kiongozi wa nchi. 
Wakati huohuo madiwani wa Busokelo walimchagua diwani wa Kata ya Kandete Salome Mwakalinga kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya halmashauri yao. 
Salome alichaguliwa kwa kupata kura 10 kati ya wapiga kura 11 waliotakiwa licha ya yeye mwenyewe kutokuwapo kwenye kikao hicho.
Chanzo: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment