MARA nyingi ni vigumu kwa mwanamke kugundua kuwa ameshika mimba katika siku za mwanzo za mtungo hadi pale atakapokosa kuoa siku zake za hedhi.
Pamoja na kwamba kuna wale ambao hasa wenye ujauzito wa kwanza na wasiojitambua hugundua wakiwa na mimba tayari ikiwa kubwa Lakini ni nadra kutokea mtu kutokua na habari kuwa ana mimba hadi anapojifungua.
Hii imekua tofauti ambapo mwanamke mmoja nchini Uingereza Clare Evance mwenye miaka24 amekutana na hali hiyo ya nadra baada ya kukaa miezi tisa na alienda kuonana na daktari wa afya akiwa na wasiwasi kuwa ana maambukizo katika figo yake.
Lakini kinyume na matarajio yake akaishia kujifungua mtoto akiwa katika chumba cha matibabu cha kitengo cha upasuaji akiwa hajui kabisa kama alikua na mimba.
“Nilipoenda kwa ajili ya upasuaji nilisikia maumivu makali sana na kwa kuwa walidhani ni maambukizi kwenye figo waliniambia niwapatie sampuli ya mkojo ndipo nilikwenda chooni lakini nikajikuta maji yanamwagika kwa mkupuo mmoja mkubwa na ndipo niliporudi na baadae madaktari wakashangaa kuona kichwa cha mtoto katika mlango wa uzazi,”Anasimulia mwanamke huyo.
Baada ya kujifungua alimpa mtoto wake jina la Erin na kusema amefarijika sana baada ya kupata msaada mkubwa wa madaktari katika kumnusuru mtoto wake.
No comments:
Post a Comment