Saturday, November 1, 2014

MAELFU WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA SENZO MEYIWA WA BAFANA BAFANA, SOUTH AFRIKA

MAELFU ya waombolezaji wamefurika katika uwanja wa Moses Mabhida uko Durban nchini Afrika Kusini ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Bafanabafana Senzo Meyiwa aliyeuawa kwa kupigwa risasi hivi karibuni
Jeneza lake liliwasili katika uwanja huo  likiwa limezungushiwa Bendera ya Afrika Kusini na likisindikizwa na viongozi mbalimbali akiwemo Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu la Afrika Kusini Danny Jordan pamoja na wachezaji klabu yake ya Orlando Pirates.
Wapenzi wa mpira wa miguu pamoja na familiya yake walionekana kutokwa na machozi  huku wakielekea  eneo maalumu ambalo lilindaliwa  kwa ajili yao.
Rais wa shirikisho la soka Afrika Kusini amesema imepoteza nyota iliyokuwa inang'aa na alikuwa msaada mkubwa kwa timu ya taifa ya nchi hiyo.
Msemaji wa Jeshi la polisi la Afrika Kusini, Bregedia Neville Malila amesema kuwa,
wamefanikiwa kumtia hatiani mshukiwa wa shambulizi hilo aliyefahamika kwa jina la Zenokuhle Mbatha mwenye umri 25 ambaye anatarajiwa kupandishwa kizimbani November 11 mwaka huu kujibu mashtaka yanayomkabili.
Senzo Meyiwa aliuawa baada ya kupigwa risasi baada ya kuwavamiwa akiwa ndani ya nyumba ya mpenzi wake Kelly Khumalos.

No comments:

Post a Comment