Friday, September 5, 2014

WAJUE WAVUMBUZI WALIOIBADILISHA DUNIA KIMAENDELEO

Bell Henry aliyetengeneza boti ya mvuke.
BELL HENRY: 
Huyu alitengeneza boti ya mvuke mwaka 1812 iliyotumika kusafiria kwenye maji. 
Mfalme wa Bahari mpaka sasa ni boti. Jiulize: Mbona shilingi inazama ikiwa kwenye maji? Katafute ni jinsi gani boti zinatengenezwa na ufumbuke kiuwerevu.
Hata huku kwetu Tanzania tuna Azam Ferry, boti zinazotupeleka Zanzibar na kwengine. Shukrani zote zimwendee mkubwa huyu aliyefariki mwaka 1830.
Maandishi kwa ajili ya wasioona yaliyogunduliwa na Braille.
BRAILLE: 
Kipofu huyu aligundua maandishi ya watu wasioona. Huyu aliubadilisha ulimwengu ‘mweusi’ na kuupa shule ya mwangaza. 
Waliopatwa na upofu baadaye hawakuwa na tatizo katika kupata digrii (shahada) hata bila ya uwezo wa kuona. Hivi sasa teknolojia hiyo inataka kuhamia kwenye simu za vipofu pia. 
Kwa kifupi, Braille alizaliwa Januari 4 mwaka 1809 na kufariki Januari 6 mwaka 1852.
Davy Humphry aliyevumbua balbu.
DAVY HUMPHRY: 
Huyu alivumbua balbu zote zinazotumika duniani kutoa mwanga wa umeme katika karne ya 18 ambapo aliunganisha waya mbili kutoka kwenye betrii mpaka kwenye ncha ya hewa ya kaboni.
Peter Durand aliyevumbua  chombo cha kuuzia vyakula kwenye makopo.
PETER DURAND: 
Huyu alivumbua chombo cha kuuzia vyakula kwenye makopo ambavyo hukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Vyakula hivyo kwa Kiingereza huitwa ‘canned food’ yaani vyakula vilivyowekwa kwenye makopo kama vile maharage, nyama, njegere, na kadhalika. 
Uvumbuzi huu ulikuwa mwaka 1810 ambapo uliwapa shida watumiaji kuzifungua bidhaa hizo kwenye makopo hayo hadi mwaka 1858 ambapo (can opener) yaani kifungulio cha makopo hayo kilipotengenezwa kwa mara ya kwanza na Ezra Warner mwenyeji wa Connecticut, Marekani.
Josephine Garis mmoja wa waliovumbua mashine ya kuoshea vyombo (dish washer).
JOEL HOUGHTON NA JOSEPHINE GARIS: 
Hawa walivumbua mashine ya kuoshea vyombo (dish washer).
COENRAAD JOHANNES VAN HOUTEN (1801-1887): Huyu ni Mdachi (raia wa Uholanzi) aliyetutengenezea mashine ya kukobolea cocoa na kuanzisha biashara ya chokoleti duniani.
Froebel ambaye ndiye mwasisi wa shule za watoto chini ya miaka mitano. 
FROEBEL, WILHELM: 
Alikuwa mwasisi wa shule za watoto chini ya miaka mitano (chekechea a.k.a shule za vidudu) huko Ujerumani.
Alifungua shule ya kwanza huko Bad Blankenburg (karibu na Keilhau) mwaka 1837. 
Hata hivyo, serikali ya Ujerumani ilizifunga shule zote za chekechea, kwa sababu zisizojuolikana, kwa miaka tisa tokea mwaka 1851 hadi 1860 ambapo ziliruhisiwa tena.

No comments:

Post a Comment