Thursday, September 4, 2014

BARUA YA WAZI : KAJALA ANGALIA YASIKUKUTE YA WEMA

Kwako Kajala Masanja. Bila shaka ni mzima wa afya. Binafsi mimi niko poa na ninaendelea na majukumu yangu kama kawaida.
Leo nimekukumbuka kupitia safu hii, nataka kuzungumza na wewe, na hasa katika suala zima la ‘ku-maintain’ ustaa wako.Ninaposema ustaa wako, namaanisha heshima, kipaji (kazi) pamoja na mapato yako.
Juzi kupitia gazeti la Ijumaa Wikienda tumeona jinsi gani umepiga hatua kimaisha. Umetoka katika maisha ya kuonekana wa kawaida, sasa unapewa heshima ambayo sidhani kama uliwahi kuitegemea kama unaweza kuipata.
Ulikuwa mtu wa karibu na aliyekuwa shosti wako, Wema Sepetu ‘Madam’ ambaye wakati huo alikuwa ana mkwanja mrefu kuliko wewe, jinsi fedha ilivyo mwana haramu kwa wakati huo ilikuwa ikiwezekana kabisa Wema akakutuma kitu, ukatii.
Jeuri ya fedha aliyoionesha Wema wakati wa matatizo yako alipokutolea shilingi milioni 13, inaonesha ni jinsi gani mwenzako alikuwa vizuri kifedha. Akakuokoa kwenye kifungo na wewe ukarudi uraiani.Unakumbuka vizuri hata baada ya yeye kukutolea fedha hizo nini kiliendelea katika maisha yenu, starehe mwanzo mwisho.
Mlikuwa mkiongozana na timu ya watu katika kumbi mbalimbali za starehe mkionesha jeuri ya fedha. Najua unakumbuka Wema alivyofanya mbwembwe na fedha nyingi kumleta msanii wa Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde kuja kuzindua filamu yake ya Super Star ambayo haijaingia sokoni hadi leo.
Kwa jeuri hiyo na nyingine nyingi alizokuwa akizifanya Madam, hakuna ambaye aliwaza kwamba siku moja ufujaji wa fedha unaweza kubadilika na kuwa fedha za mawazo.Hakuna aliyewaza kwamba wewe ambaye ulikuwa chini yake ungeweza kuja kuwa juu yake.
Hakuna linaloshindikana chini ya jua na sasa kibao kimegeuka, sasa fedha imekutembelea.Heshima ile ambayo alikuwa akiipata aliyekuwa shosti wako, unaipata wewe.Hapo ndipo unapotakiwa kupatazama kwa makini.
Kama umefanikiwa kufungua kampuni yako ya kuzalisha filamu, iwekee misingi thabiti isije kuyeyuka kama ilivyoyeyuka ya huyo aliyekuwa shosti wako (Wema).Tengeneza mazingira ya kuzalisha kazi na kuziuza kweli Watanzania waone kwamba kuna filamu bora zinazalishwa kutoka katika kampuni yako.
Kuwa na fedha nyingi na kutokokuwa na mipango mipya ya kuzizalisha, ni rahisi kupotea na kurudi kule ulikotoka.Njia aliyopitia aliyekuwa shosti wako iwe funzo kwako. Chagua njia sahihi ili uendelee kuwa makini katika maisha yako.
Asikwambie mtu, starehe za kupindukia huku ukiamini ‘bado zipo benki’ ndiyo chanzo cha wengi kuporomoka.Natumai sijachelewa kuzungumza na wewe maneno haya machache, yafanyie kazi ili usije kujifunika shuka wakati kumekucha. Mungu akubariki!
Chanzo: GPL

No comments:

Post a Comment