SHIRIKA la ndege la Australia linalofahamika kama Qantas limeanza
kurusha ndege yake ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi ya abiria duniani na
inayofanya safari zake kwa umbali mrefu zaidi.
Ndege hiyo iliyotwa kama Airbus A380 ilitua katika uwanja wa
kimataifa wa Dallas-Fort Worth saa 15 tangu ilipoondoka Sydney,
Australia safari ya Kilometer 13,805 ikiwa na abiria 480.
Uwanja wa
kimataifa wa Dallas- Fort Worth ni uwanja mkubwa wa ndege unaounganisha
ndege zote za Marekani na Latin America. Uwanja huo umeonekana kufaa
zaidi kwa ndege hiyo.
Angalia picha za ndani:
No comments:
Post a Comment