Saturday, August 2, 2014

EVRA AFICHUA SIRI NZITO ZA KLABU AISALITI MAN UTD

SIKU moja baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari mjini Turin nchini Italia, beki wa pembeni kutoka nchini Ufaransa Patrice Evra, amepasua ukweli wa mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati yake na viongozi wa klabu ya Man utd.
Evra amesema viongozi wa Man utd wakiongozwa na meneja mpya wa klabu hiyo Louis van Gaal waliwa wakimbembeleza ili aendelee kusalia Old Trafford, lakini hakukubaliana na ombi hilo na badala yake alihitaji kutimiza lengo lake la kucheza soka nje ya nchi ya Uingereza. 
Amesema pamoja na yote hayo kutokea, bado ofa ya klabu ya Juventus ilipowasili mjini Manchester, ilikuwa ikiundiwa mikakati kwa ajili ya kuwekewa vikwazo lakini mwisho wa yote ilikuwa vigumu kwa viongozi wa Man utd kufanya hivyo. 
"Manchester United waliweka vipingamizi vya kila aina ili nibaki na waliniahidi kunipa nafasi ya unahodha lakini nilionyesha ukakamavu kwa kufanya maamuzi magumu na kuwaambia nataka kuondoka” Evra amekiambia kituo cha televisheni cha Sky Sports. 
"Van Gaal hakupendezwa na hatua ya kuondoka kwangu Old Trafford, na yeye alikuwa mstari wa mbele kuwashawishi viongozi wengine ili niendelee kubaki klabuni hapo, lakini tayari nilikuwa nimeshafanya maamuzi kwa kuichagua Juventus.” 
Amongeza Evra. Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 33, amesema ni vigumu kufanya maamuzi ya kuachana na klabu kama Man Utd kutokana na mazuri yaliopo kwenye klabu hiyo, lakini akasisitiza uwepo wa uziri kama huo huko Juventus Stadium imekuwa sbabu kubwa ya kuondoka na kutua mjini Turin.
 Patrice Evra, tayari alikuwa meshatangaza msimamo wa kuachana na Man Utd tangu kati kati ya msimu uliopita, huku lengo lake kubwa likuwa ni kuhitaji mazingira mapya ya kucheza soka lake.
Evra amekabidhiwa jezi namba 33 na uongozi wa klabu ya Juventu

No comments:

Post a Comment