STAA wa kike wa filamu bongo, Aunt ezekiel, ambaye ni shoga mkubwa wa miss tanzania 2006 wema sepetu ameibuka na kutamka bayana yeye si mpambe wa mrembo huyo, wala sio mbeba mikoba wake na wala haishi kwa kusubiri pesa zake anazohongwa na Diamond.
Staa huyo alifunguka kuwa yeye hausiki na kumpeleka mwenzake kwenye starehe kwani wote huenda kwa matamanio yao binafsi, Aunt aliwaponda wote waliokuwa wakimuhusisha na kauli ambayo ilitolewa na Diamond kwamba wema anapotezwa na mashoga zake wapenda starehe.

"wajinga wakubwa, watu wananihusisha mimi na masuala ya wema na Diamond. Mimi ni staa mkubwa na wema ni staa , nimeanza kuhangaika na maisha mda mrefu sio mpambe wa wema , kwanza ana nini cha ziada cha kunipa hadi niwe mpambe wake?
Nina maisha yangu na miradi yangu toka kitambo, kama kwenda kwenye starehe wema anaenda kwa matamanio yake na mimi na matamanio yangu, siishi kwa sababu ya pesa za diamond wala wema, masuala yao ya mapenzi hayanihusu kabisa, wayaongee wayamalize kama kuchukua hatua wachukue sio kuongelea pembeni, mimi sibembelezi urafiki kwa sababu ninayamudu maisha na ni STAA.
Tena ole wao wanaonijua aunt na mihangaiko yangu siwezi kufikiria ujinga huo, sitegemei hela ya wema wala diamond wake, wakome kabisa tena wanikome na iwe mwisho" Alisema staa huyo aliyefanya vizuri kwenye movie ya Young billionaire.
No comments:
Post a Comment