Thursday, July 10, 2014

"UHARAMIA UNAWEZA KUPUNGUA SOMALIA" YAFAFANUA RIPOTI YA OXFORD NA KING'S COLLEGE

UTAFITI wa hivi karibuni unaashiria kwamba uharamia kutoka pwani ya Somalia huenda ukapungua kwa kiwango kikubwa kwa kuwapatia wazee wa koo za kisomali njia mbadala za kujikimu kimaisha.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford na King's College mjini London, iliyochapishwa katika jarida moja la Uingereza, Jamii huwalinda maharamia wakati hawana njia nyingine za kujipatia kipato.
Kwa sasa Jamii ya kimataifa inategemea mikakati iliyo ghali mno, zikiwemo meli za kijeshi kuzuia uhaharamia wa majini na kuweka njia za safari za majini kuwa salama .
Lakini utafiti huu unakubaliana na yale ambayo yamekuwa yakipendekezwa na wadau mbalimbali Afrika mashriki, kwamba suluhu la kudumu ni kujenga miundo mbinu kama vile bandari na barabara zitakazo wawezesha wanavijiji wa koo mbalimbali wanufaike kwa fursa za kibiashara halali, zitakazowawezesha kupata tiza za kuendeleza maisha yao.
Watafiti wamebaini maeneo meli zilikotekwa nyara kote bahari ya Somalia
Mwandishi wa utafiti huo anasema awali watunga sera wameazimia zaidi kutafuta kiini na vichochozi vya uharamia wa baharini pasi na kuchunguza ni kwa nini wanalindwa na jamaa zao na viongozi wa mbari zao.
Watafiti hao wameweza kubaini maeneo meli zilikotekwa nyara kote bahari ya Somalia, na wakitumia data walizozopata kutoka kwa Benki ya dunia , walifanya mahojiano na wakazi wa sehemu hizo.
Uharamia umekithiri katika maeneo maskini huku
ikibainika wazi kwamba uharamia umeenea zaidi katika maeneo ambayo yamefungiwa kufikia njia za barabara za kibiashara hasa zinazoelekea bandarini, kwa mfano maeneo yanayozozaniwa huko Puntland na Somalia ya kati.
Wakagundua pia kuwa katika yale maeneo ambako wakaazi wanaendendeleza biashara halali ama kwa kutoza kodi , kwa kuingiza au kuuza bidhaa nje ya nchi, kupitia bandarini kamwe hawamlindi haramia wa baharini.
Katika maeneo maskini na vitongoji duni, ilionekana mtindo wa visa vya uharamia wa majini na utekaji nyara meli, kuongezeka kila wakati wa upigaji kura za mitaani humo, kumaanisha tabia hiyo si tofauti na za wanasiasa.
Kwa mfano uitaliano na Taiwan walio na mtindo wa kuwalinda wahalifu kwa lengo la kupata fedha kwa njia haramu zitakazowanufaisha katika malengo yao ya kutwaa madaraka ya kisiasa.
Mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo Federico Varese, kutoka chuo kikuu cha Oxford Uingereza amesema jamii hizo huwalinda maharamia wa majini wakati hamna namna nyengine ya mapato mazuri.
Huku mwandishi Dr Anja Shortland,wa chuo kikuu cha Kings London, akajumuisha kuwa itabidi suluhu la uharamia wa majini lipatikane ardhini kwa maana kuwa kama vile benki ya Benki ya dunia inavyopendekeza, kuwe na mkataba wa kuweka mfumo thabiti wa kisiasa utakaofanikisha maendeleo ya kijamii.

No comments:

Post a Comment