Thursday, July 3, 2014

TLS KUISHTAKI SERIKALI YA TANZANIA

Na Mwandishi wetu
CHAMA cha Wanasheria Tanganyika(TLS), kinatarajia kufungua kesi katika mahakama kuu kuishitaki serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa maamuzi yake ya kuunga mkono usitishaji wa mahakama ya jumuiya ya nchi za kusini mwa afrika (SADC Tribunal).
Maamuzi hayo yametangazwa na mjumbe wa kamati ya haki za binadamu wa chama hicho, Daimu Khalfan katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwao jijini Dar es Salaam. 
Khalfan alisema kwenye mkutano wao wa kilele uliofanyika Windhoek, Namibia, Agosti 17 2010, viongozi wa Jumuiya ya nchi wanachama Tanzania ikiwemo wamlifanya maamuzi ya kusitisha mahakama hiyo ambako Agosti 2012 kwenye mkutano wao wa kilele huko Maputo waliamua kuiua kabisa na kuitangaza kama mahakama ya kikanda.
Akifafanua zaidi kusudio hili alisema kwa hatua hiyo sasa itaifanya mahakama hiyo kazi yake kuwa kutafsiri miakataba na protokali zinazohusiana na migogoro miongoni mwa nchi wanachama pekee na hivyo kuzuia raia kupata haki ambayo pengine wasingeweza kuipata katika nchi zao.
Kwa mujibu wamjumbe huyo TLS wanaona hatua hiyo ni kurudisha nyuma mchakato wa kuimarisha utawala wa sheria , kuheshimu utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na ufikiaji wa haki kwa raia wa nchi wanachama. 
Pia alisema wanaona hali hii ni sawa na kuvunja mkataba wa uwanzishaji wajumuiya hiyo ambako miongoni mwa vipengele vya mkataba wake ni kuimarisha amani na utawala bora na bila uwepo wa mahakama huru ni wazi kwamba hakuna utawala bora. “TLS inataka kuona mahakama hii ikirudishiwa mamalaka yake na nguvu za kisheria ilizokuwa nazo awali,”alisisitiza Khalfan. Kwa upande wake mjumbe wa chama hicho, Steven Axwesso, alisema tangu wapate tetesi za kutaka kufungwa kwa mahakama hizo juhudi mbalimbali zilifanywa na mashirika katika kuhakikisha haifungwi kwa njia ya diplomasia lakini ilishindikana ndio maana hii leo wameamua kufungua kesi wakiamini haki itapatikana huko.
Axwesso alisema chanzo cha kufikiwa hatua hiyo kilitokana na kesi walioshinda wawekezaji walionyangaywa mashamba yao nchini Zimbabwe na hivyo viongozi wengine wanahofia yasije yakawakuta. 
Baadhi ya athari ambazo zimeanza kujitokeza alisema ni pamoja na mashauri mbalimbali ambayo tayari yamefunguliwa hayataweza kusikilizwa tena na kwa yale yanayotarajiwa kupelekwa haitawezekana. 
Wakati kwa upande wa uongozi tayari Rais wa mahakama hiyo ameshasimamishwa kabla ya kufikisha mkataba wake wa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment