BAADA ya kushuhudia kalamu ya magoli kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia kati ya Brazil na Ujerumani, imepigwa nusu fainali ya pili kati ya Argentina na Uholanzi.
Matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Sao Paolo ni ushindi uliotokana na mikwaju ya penati wa 4-2 kwa Argentina.
Mechi hiyo ilikuwa ya kukamiana na kucheza kwa kujihami kwa timu zote mbili iliisha kwa sare tasa katika dakika 120 na hivyo ikaamuriwa ipigwe mikwaju ya penati.
Waliopata penati kwa Argentina ni Messi, Aguero, Garay, na Rodriguez wakati Robben na Dirk Kuyt wakifunga penati mbili za uholanzi huku Vlaar na Sneijder wakikosa.
Argentina sasa itaenda kucheza na Ujerumani fainali jumapili hii, wakati Uholanzi wakikutana na Brazil jumamosi kugombea medali ya mshindi wa 3.
Kichwa kwa kichwa: Ezequiel Garay na Robin van Persie waligongana
Arjen Robben alikaziwa vibaya sana, lakini alionesha cheche kama kawaida
Nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie akijaribu kuupiga mpira kwa guu lake la kulia.
Georginio Wijnaldum na Javier Mascherano mambo hayakuwa rahisi.
No comments:
Post a Comment