Friday, July 4, 2014

HARVARD CLUB OF WASHINGTON WALIPOTEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Harvard Club Of Washington, Bi. Caren A. Pauley akiutambulisha umoja wa wanafunzi waliowahi soma Chuo Kikuu cha Harvard waishio Washinton Metro Area kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula siku ya Jumatano July 2, 2014 umoja huo ulipotembelea Ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya kukutana na jumuiya mbalimbali za Kitanzania na Taasisi zinazoshughulika na maswala ya Tanzania na kuweza kuongea pamoja kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Afisa Immaculata Diyamett anayeshughulikia masuala ya Utalii kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, akiwakaribisha wageni wote Tanzania House na kuwaambia wajisikie wapo nyumbani.
Rais wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard Club Of Washington, Bi Yi-Fun Hsueh ambaye pia ni mmoja ya waratibu akiongea machache na kumshukuru Balozi Liberata Mulamula kwa kukubali kuwakaribisha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuja kukutana na Jumuiya za Kitanzania na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kujuana na kubadilishana mawazo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekanai Mhe. Liberata Mulamula akiwakaribisha Umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Cha Harvard waishio Washinton Metro Area kikundi kinachobeba jina la  Harvard Club of Washington kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kuwaelezea kuhusu Tanzania na vivutio vyake chini ni maelezo aliyokuwa akitoa Mhe. Balozi.
BOFYA KUMSIKILIZA HAPA!!!
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi toka kwa Rais wa Umoja huo Bi. Yi- Fun Hsueh.
Rais wa Umoja huo Bi. Yi- Fun Hsueh akipokea zawadi toka kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Juu na chini Harvard Club Of Washington na wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Balozi Libarata Mulamula.
Mchapalo ukiendelea...

No comments:

Post a Comment