Friday, July 4, 2014

BAADA YA MY NUMBER ONE SASA DIAMOND ATUHUMIWA KUIBA TENA WIMBO WAKE MPYA WA MCHIRIKU 'MDOGO MDOGO'

MALALAMIKO ya baadhi ya wasanii kuibiana kazi yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwa wasanii wachanga au wasiokuwa na majina kuwalalamikia wasanii wenye majina makubwa tena wanapokuwa na wimbo uliofanya vizuri na kubamba katika vituo mbalimbali vya redio na Tv.
Kwa upande wa Msanii anayevuma kila kona ya Tanzania na nje ya mipaka ya nchi, Diamond, yeye amelalamikiwa mwishoni mwa maka jana na mwanzo mwa mwaka huu, na msanii wa kike Dyna baada ya kutoka na wimbo wa My Number One, ambao Msanii Dyna alidai kuwa ameibiwa na Diamond.

Msanii Diamond baada ya kuachia song hilo la My Number One lililopata kubamba vilivyo ndani na nje ya nchi, ndipo Dyna aliibuka na kudai kuwa song hilo lilikuwa ni lake na kuachia Song lake ambalo pia lilikwenda kwa jina hilo hilo likiwa na midundo sawa na My Number One wa Diamond.

Baada ya wasanii hao kuvutana na kushutumiana sana kazi ilibaki kuwa kwa mashabiki wao ambao ama kwa hakika siamini kama yupo hata mmoja ambaye alipata jibu la kujiridhisha kuwa wimbo huo ulikuwa ni haki ya nani kati yao na hatimaye suala hilo likazimika kimya kimya huku song la Diamond likiendelea kutamba na la Dyna likipigwa kwa chaaati na leo zote mbili hazisikiki tena kama ilivyokuwa awali na wakati wakigombea wimbo huo.

Haijapita muda mrefu tangu kuibuka kwa sakata hilo la Dyan na Diamond, na sasa limeibuka jingine baada msanii aliyeibukia BSS siku za nyuma, Wababa ambaye naye pia ameibuka baada ya kuanza kutamba kwa song jipya la Diamond, lenye miondoko Mchiriku linalokwenda kwa jina la Kitorondo au Mdogo mdogo.

Mara tu baada ya kutoka wimbo huu zilivuma stori kuwa Diamond amemuigilizia msanii mwenzake Ally Kiba na mdogo wake waliotoka na wimbo kama huo na unaoendana na miondoko hiyo hiyo, ambapo haikuweza kufahamika kuwa ni nani aliyemkopo mwenzake kwani Diamond alianza kusikika wa kwanza na baadaye Kina Kiba na mdogo wake ambao walisema kuwa wao walishaurekodi siku nyingi tu wimbo huo ila walichelewa kuuachia.

Jibu la nani kakopi wanalijua wenyewe kuwa ni nani aliumiza kichwa kutunga na kupangilia muziki na nani amepita 'shot cut' kwa kukopi na kupesti.
Lakini kubwa zaidi ni wimbo huo huo, ambao umeelezwa kuwa ni wa msanii Wababa, aliyeeleza kuwa wimbo huo ni wake na alishawahi kuurekodi akiwa na Msanii Asley siku za nyuma.
Msanii huyo aliyewahi kushiriki katika shindano la Bongo Star Search (BSS) , Wababa amewatuhumu maswaiba wa ‘Muziki Gani’ Nay wa Mitego na Diamond Platinumz kwa kumuibia kazi zake kwa nyakati tofauti.

Akizungumza wakati wa mahojiano na kipindi cha 'Friday Night Live' ya East Africa TV, Wababa alisema kuwa Diamond amemuibia wimbo wake ambao alikua anauita ‘Kitorondo’ na kwamba aliubadilisha jina baadae.
''Kiukweli kuhusu Diamond, mimi mwenyewe nimetumiwa hiyo ngoma ambayo ameitoa, nimeiskiliza jinsi ilivyo kuanzia idea, mwendo, style kiukweli ni kazi yangu ile ile ambayo ameibadilisha jina tu badala ya Kitorondo na kuwa mdogo mdogo, huku Kitorondo ikibaki katika mistari ya kuimba''. alisema Wababa
Wababa alisema kuwa wimbo huo baada ya kuurekodi aliuweka katika mitandao ya kijamii mwezi mmoja uliopita. 

Aidha Wababa alisema kuwa baada ya kuusikia tu alishindwa kulalamika kwa haraka baada ya kumsikia Diamond pia akijihami kuwa wimbo huo umevuja kabla ya kuuachia.
''Kwa hiyo sikuona sababu ya kuongea kitu kwa sababu haikuwa official''. alisema Wababa.
Alipoulizwa ni wapi ambapo Diamond aliusikia wimbo huo, amesema huo ni wimbo wake alioutoa miaka minne iliyopita akiwa na Dogo Asley na aliuweka kwenye mtandao wakati anatumia jina la Nurdi, kabla hajaanza kutumia jina la Wababa aliposhiriki BSS. “Ni nyimbo ambayo iko mtaani na watu wengi wanaielewa. 

Kwa upande mwingine, Wababa amedai kuwa alifanya kazi na Nay wa Mitego katika studio za Mazoo lakini baaadae Nay alirudi studio na kuongea na Mazoo kutaka kuununua wimbo huo kwa shilingi milioni moja bila kumshirikisha Wababa.
“Hivi karibuni nimefanya ngoma mpya na Nay wa Mitego, ni ngoma ambayo ilikuwa iko paid kwake pamoja na studio. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba siku mbili baada ya kufanya kazi nikapigiwa simu na producer akiniambia kwamba jamaa amerudi tena kwa ajili ya kutaka kununua wimbo kwa milioni moja, auchukue wimbo aende akaufanye sehemu nyingine. 
Baada ya hapo hata mahusiano yangu na mshikaji yamekuwa sio mazuri. Ukimpigia simu anakwambia yuko busy kuna kazi anafanya atanicheki, hadi kufikia leo sielewi.” alisema Wababa

Watuhumiwa hao wote walipotafutwa kwa njia ya simu kipindi kikiwa hewani simu zao hazikuweza kupatikana.
Diamondi hivi sasa yupo mbioni kukamilisha wimbo wake mpya ulio katika miondoko ya Taarab, ambao pia atauachia siku chache zijazo, sasa baada ya kuachia wimbo huo siju lipi tena litaibuka. 
MASHABIKI YETU MACHO.

No comments:

Post a Comment