Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora.
Mara nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia A’level, Hawa wengine walikua wapo shule
wakisoma na kuishi vizuri.
Hawa ni baadhi ya watoto wakishua ambao kwasasa ni celebrities wetu…
****************
VANESSA MDEE
Vanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu) ambaye alikua ni mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia.
Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani.
Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.
*********************
NISHER
Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha.
Nisher amekulia katika maisha mazuri na hadi ni wakishua bado.
Baba yake aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.
***************
JOKATE MWEGELO
Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini.
Kumbuka Jokate alizaliwa washington DC nchini Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko.
Alipomaliza high school katika shule ya Loyola ndipo alipogombania Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2.
*****************
LUCCI
Jina lake halisi anaitwa Luciano Tsere au unaweza kumuita Lucci ambaye ni producer maarufu nchini. lucci amezaliwa tarehe 30 September mwaka 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao.
Lucci naye kama jokate amekulia Obey kwenye familia bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment