MSHAMBULIAJI matata wa timu ya soka ya Uruguay Luis Suarez anakabiliwa na marufuku ya mda mrefu itakayomlazimu kukosa mechi nyengine za michuano ya kombe la dunia iwapo atapatikana na hatia ya kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.
Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha harakati za kumuadhibu mcheza huyo kufuatia ushindi wa moja kwa bila dhidi ya Italy siku ya Jumanne.
Chiellini amedai kwamba Suarez alimng'ata bega lake licha ya Suarez kudai kuwa ni mchazaji huyo aliyemchezea vibaya.
Suarez na Chiellini

Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akapigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi 24 ama miaka miwili.
Refa aliyesimamia mechi hiyo kutoka Mexico Marco Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kisa hicho,lakini FIFA bado inaweza kumuadhibu Suarez.
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Liverpool Jan Molby anatarajia kwamba Suarez atapigwa marufuku kwa mechi zote za kombe hilo zilizosalia.
Raia huyo wa Denmark ameliambia gazeti la Liverpool la Echo kwamba '' nina hakika FIFA itachukua swala hilo la Suarez kama mfano kwa wengine''.
''Ni dhahiri kwamba matumaini yake ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia iliosalia yamekwisha na ninataraji kwamba FIFA itampatia marufuku ya mda mrefu''.
Chanzo: BBC Swahili

No comments:
Post a Comment