Upande wa
pili wa shilingi! Kwa mara ya kwanza tangu ahusishwe na skendo ya
ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17, mume wa mwimbaji wa Injili
nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameibuka na kuzungumza na Uwazi
katika mahojiano maalum dhidi ya kashfa yake hiyo huku akitishia kujiua.
Akizungumza
kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa moja mwishoni mwa wiki iliyopita huku
akikanusha kukimbilia mafichoni baada ya kuondoka nyumbani kwake
Tabata-Kimanga, Dar hivi karibuni, Mbasha ambaye pia ni mwimba Injili
kama mkewe, alianika kila kitu akidai cha siri kwamba anajua anachezewa
mchezo mchafu baada kuwepo kwa gogoro zito kati yake na mkewe hadi
kutishia uhai wa ndoa yao.
ASIMULIA TUHUMA
“Tuhuma
zilizoripotiwa na binti aitwaye... (anamtaja jina) ambaye kweli ni ndugu
wa mke wangu (Flora) kwenye Kituo cha Polisi Tabata-Shule (Dar) si za
kweli.
“Anayefanya mambo hayo yote ni mke wangu, anataka nipotee ili awe huru. Mimi najua hilo.”
KASHFA YA KUTENGENEZA
“Hii kashfa ni ya kutengeneza ili nipotee lakini sipo tayari kupata aibu, bora nijiue.
“Mke wangu amekuwa tatizo kwenye ndoa yetu.
“Kweli ndoa
yangu na Flora ina matatizo lakini matatizo yetu ya ndani sana hakuwa na
sababu ya ‘kuinjinia’ mpango mchafu wa kunimalizia gerezani mimi ili
yeye aponde raha.
“Nyuma ya haya mambo kuna vitu mtu ukivisema ni aibu sana kwa upande wa pili. Lakini navijua.”
MKE ALIONDOKA NYUMBANI
“Mke wangu
aliondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini. Hebu fikiria hapo. Mwanzo
alianza kwenda ‘gym’ saa 11:00 alfajiri na kurudi saa 4:00 asubuhi. Pia
saa 10:00 jioni aliondoka tenda kwenda gym akawa anarudi kati ya saa
3:00 hadi 4:00 usiku.
“Nilipomuuliza
alinijibu kuwa ni kwa sababu anatembea umbali mrefu. Hebu ona sababu
ilivyo dhaifu jamani! Hata kama ungekuwa wewe mwandishi, unaonaje?”
“Mimi ni mtu maarufu, ningetaka mwanamke ningepata, iweje nibake?
“Jaribu
kufikiria, katika tatizo kubwa kama hili ambalo linaweza kunifanya
nifungwe, nilitarajia mke wangu awe upande wangu, lakini cha ajabu yeye
ndiye amekuwa nyuma ya adui zangu, niamini nini mimi zaidi ya yeye
kuhusika na kuniangamiza?”
“Hausigeli wangu ni mzuri, kwa nini nisimbake yeye?”
AFUATILIA
“Nilipofuatilia
niligundua tayari kuna tatizo kwenye ndoa yetu. Mdudu alikuwa ameingia
ndani ya ndoa kwani hadi sasa mke wangu siishi naye. Anaishi hotelini.
“Anachokifanya
mke wangu ni kitu kibaya mno. Alimtengeza yule binti ambaye nilikuwa
namsomesha sekondari pale (anataja shule maarufu Dar), akampa semina ya
kutosha kwamba aseme nimembaka ili nipate misukosuko na yeye awe huru.
“Kama hiyo
haitoshi, akala dili na madaktari, wakafoji majibu ya vipimo vikionesha
kweli yule binti ameingiliwa, sasa sijui kama vipimo vilioneshaje kama
ni mimi.
“Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia kuona napandishiwa kizimbani kwa jambo la kutengenezewa.
“Napiga
picha nitakapofikishwa mahakamani jinsi ambavyo vyombo vya habari
vitakavyoandika na picha zangu kwa kesi ya ubakaji ambayo si ya kweli.
“Dah!
Inaniuma sana. Mke wangu nimemfanyia vitu vingi sana. Hakustahili
kunitendea ubaya huu. Alikuwa hafahamiani na mtu yeyote mkubwa. Mimi
ndiye nimempeleka kwa watu wakubwa wakamsaidia sasa amenigeuka, siamini.
Narudia tena, heri kufa kuliko fedheha hii,” alisema Mbasha kwa
uchungu.
HAYUKO MAFICHONI
Kuhusu kuwa
mafichoni, Mbasha alisema: “Sipo mafichoni, sijaambiwa na mtu yeyote
nikatoe maelezo polisi. Nipo nimejaa tele, nikiambiwa nahitajika
nitakwenda kutoa maelezo yangu kwani sijawahi kutenda kosa hilo na Mungu
awe shahidi yangu.”
Kamanda wa
Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Dar, Marietha Minangi alithibisha kuwepo kwa
ishu hiyo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.
Flora na
Mbasha walifunga ndoa Agosti 22, 2002 hivyo mwaka huu wametimiza miaka
12 wakiwa pamoja ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Elizabeth.
Kwa hisani ya Lindi yetu
Kwa hisani ya Lindi yetu
No comments:
Post a Comment