Nasrah Rashid (kulia) enzi za uhai wake. Kushoto aliyekaa ni baba yake mzazi Rashid Mvungi.
Habari
zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mtoto Nasrah Rashid (4)
aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua
na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki
dunia.
Nasrah
alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi
wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama
yake mzazi kufariki.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU NASRAH MAHALI PEMA PEPONI.
AMINA.
No comments:
Post a Comment