Monday, June 30, 2014

ISIS YATANGAZA UTAWALA WAO

Mpiganaji wa kundi la ISIS linalodai kutangaza taifa la kiislamu.
NCHINI Iraq hali inaendelea kuzorota, raia wakiendela kukimbia mapigano .
Sasa wapiganaji wa kiislam wa Kundi la iSIS wamesema kuwa wanataka kuweka utawala wao baada ya kudhibiti maeneo ya Iraq na Syria
Msemaji wa wanamgambo hao wa kiislamu wa ISIS ametangaza kuwa wataunganisha ardhi wanazozidhibiti walizoziteka kutoka Iraq na Syria ndio waunde eneo moja wanalolitaja kama 'Islamic Caliphate' litakalotawaliwa na sheria kali za kiislamu.
Kama vile ilivyotolewa taarifa ya Shami ndivyo ilivyotangazwa kauli ya Shaykh Abu Muhammad al-Adnani, kupitia mtandao wa You Tube.
ISIS wameteka maeneo Iraq na Syria. Serikali ya Iraq ina wakati mgumu kukabiliana nao.
Ameendelea kusema eneo hilo litajumuisha tangu Aleppo huko Syria hadi Diyala mashariki mwa Iraq.
Na kufuatia hali hiyo msemaji huyo amefafanua kwamba sasa kundi hilo badala ya kuwa na kujulikana kwa jina la ufupi ISIS na the Levant sasa watajiita tu "the Islamic State" Taifa la kiislam.Kundi hilo pia limesema limemteua kiongozi wao -- Abu Bakr al-Baghdadi -- kama 'Caliph', wakidai ndio kiongozi wa waslamu wote.Haya yote yanatangazwa baada ya kundi hilo la Isis kupata mafanikio makubwa katika vita vivyo.Wakati huo huo Serikali ya Iraqi imesema vikosi vyake vimepiga hatua kuelekea Tikrit, mji wa kazkazini mwa nchi hiyo uliotekwa na wanamgambo hao wa kiislamu zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Msemaji wa jeshi la Iraqi Luteni jenerali Qassim al-Moussawi amesema jeshi lao liko katika awamu ya kwanza ya mapigano hayo ya tangu alhamisi.
Televisheni ya kitaifa ilionesha helicopters zikishambulia maeneo kadhaa huko jangwani lakini hamna ushahidi kamili wa kuaminika kwamba wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuingia mjini.Waasi hao wametega mabomu kando kando mwa barabara kuu kujaribu kuzuia vikosi vya serikali.Hata hivyo mwandishi wa BBC aliyeko Baghdad amesema hii ndio hatua ya kwanza thabiti iliyowahi kuchukuliwa na serikali dhidi ya ISIS tangu waasi hao walipoanza kushambulia na kuyateka maeneo ya nchi hiyo kwa kasi iliyowashangaza wengi.

No comments:

Post a Comment