Sunday, May 25, 2014

VURUGU ZATAWALA KATIKA NGUMI MSHINDI ASHINDWA KUTANGAZWA

Bondia Said Mbelwa kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa UBO uliofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam hata hivyo mshindi ajapatikana kutokana na fujo zilizotokea katika raundi ya nane picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Zumba Kukwe kushoto akioneshana umwamba na Josef Njelekela wakati wa mpambano wao waliotoka droo picha na  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Zumba Kukwe kushoto akioneshana umwamba na Josef Njelekela wakati wa mpambano wao waliotoka droo picha na  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpongeza khalid chokolaa baada ya kuibuka mshindi katika mpambano wake
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpongeza khalid chokolaa baada ya kuibuka mshindi katika mpambano wake
Bondia Tasha Mjuaji kushoto akipambana na Rajabu Mahoja wakati wa mpambano wao

Bondia Mada Maugo kushoto akiwa anapigana na Thomas Mahali mwenye rasta
Bondia Mada Maugo akiwa anazipanga kavukavu na bondia Thomas Mashali walipiokutana katika ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ubingwa wa UBO umekosa kutangazwa mshindi mbele ya mashabiki baada ya vurugu kubwa kutokea katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
ubingwa huo uliokuwa ukigombaniwa na mabondia Said Mbelwa na Karama Nyilawila alishindikana kupatikana mshindi baada ya raundi ya nane bondia Karama kumpiga kichwa Mbelwa cha wazawazi na kusababisha Mbelwa kuamaki kwa kulipiza kisasi na kumsukuma nje pia kumrukia kama ninja wakati alipotoka nje ya uwanja mpambano huo wa raundi kumi ulijikuta ukishia kwa raundi nane

na refarii pamoja na majaji wake kukimbia ukumbini wakiwaacha mashabiki bila kureta majibu ya mpambano huo hata hivyo mbelwa alirudi uringoni kwa ajili ya kuenderea kupambana na mpinzani waka alikimbia moja kwa moja kutokana na kuona kihama cha ngumi za mtaani zilivyuoanza
wakati huohuo bondia Mada Maugo alimpiga mwenzake Thomas Mashali kwa ngumi tatu mfululizo kavuvu 
bila kufata sheria ambapo ni kinyume na taratibu za mchezo wa masumbwi duniani kote mabondia hawo ambao wote walionekana wamelewa walipishana kiswahili mbele ya promota Ally Mwazoa ambaye ame haidi kabla ya kumaliza mwaka mabondia hawo wawe wameshapanda uringoni 
ambapo mpambano wao wa kwanza Thomas Mashali alimgalagaza kwa point Mada Maugo
katika mapambano ya utangulizi yaliyochezwa siku hiyo bondia Khalid Chokoraa ambaye ni mwanamuziki alimpiga kwa k,o ya raundi ya kwanza  Abdul Manyenza na Mwaite juma alimpiga Athumani Rashid wa Tanga kwa point wakati Selemani Galile alipigwa kwa point na Abdalah Pazi

No comments:

Post a Comment