Thursday, May 29, 2014

TANZANIA YAAHIDI KUPEKELEKA WANAJESHI ZAIDI KWENYE NCHI ZENYE MIGOGORO AFRIKA

Baadhi ya viongozi mbalimbali wakisikiliza wimbo wa taifa katika maadhimisho hayo ya kuwakumbuka wanajeshi waliopoteza maisha kwa kulinda amani
Baadhi ya viongozi mbalimbali wakisikiliza wimbo wa taifa katika maadhimisho hayo ya kuwakumbuka wanajeshi waliopoteza maisha kwa kulinda amani.
Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Jeshi la Kulinda amani la Umoja wa Mataifa yamefanyika leo jijini Dar Es Salaam, huku kukiripotiwa jumla ya wanajeshi 106 wamepoteza maisha mwaka jana kati ya hao askari 10 kutoka nchini Tanzania na kuongeza idadi ya vifo kufikia wanajeshi 3200 toka kuanza kwa shughuli za kulinda amani.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi ya Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi alisema kuwa, wataendela kutoa bataliani ya wanajeshi wa kulinda amani katika nchi zenye migogoro, lengo ni kusaidia kutuliza amani pamoja kukomesha unyanyasaji na ukatili kwa wanawake na watoto.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Jama Gulaid akiweka shada la mauwa kama kumbukumbu ya kuwakumbuka wanajeshi waliopoteza maisha kwa kulinda amani katika nchi zenye vurugu.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Jama Gulaid akiweka shada la maua kama kumbukumbu ya kuwakumbuka wanajeshi waliopoteza maisha kwa kulinda amani katika nchi zenye vurugu.
Dkt. Mwinyi alisema kuwa maadhimisho hayo yanawapa fundisho na muungozo wa kuendelea kulinda amani ya nchi yetu ili isiwe na matatizo kama wanayopata nchi jirani.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Taifa nchini Dkt. Jama Gulaid ambaye pia ni mwenyeji katika maadhimisho hayo alifafanua kuwa, jumla ya wanajeshi wapatao116,000 duniani kote wamesambazwa katika nchi zaidi ya 120 pamoja na vituo 16 vya kutuliza amani.
Baadhi ya Polisi walishiriki katika kulinda amani hawakubaki nyuma katika maadhimisho hayo nao waliwatumbuiza watanzania kwa nyimbo ya amani.
Baadhi ya Polisi walishiriki katika kulinda amani hawakubaki nyuma katika maadhimisho hayo nao waliwatumbuiza Watanzania kwa nyimbo ya amani.
Wanaishukuru serikali ya Tanzania kuendelea kutoa wanajeshi wa kulinda amani sehemu mbalimbali ambazo kuna machafuko.
Kauli mbiu ya mwaka huu ulinzi wa amani wa umoja wa mataifa, jeshi la amani, jeshi la mabadiliko na jeshi la siku zijazo.

No comments:

Post a Comment