ATLETICO Madrid ndio mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Hispania, ukipenda unaweza kuiita La Liga baada ya kulazimisha sare ya 1-1 usiku huu na Barcelona Uwanja wa Camp Nou.
Hilo linakuwa taji la 10 la Atletico la La Liga, baada ya awali kutwaa katika misimu ya 1939–40, 1940–41, 1949–50, 1950–51, 1965–66, 1969–70, 1972–73, 1976–77 na 1995–96.
Aidha, hii inakuwa mara ya kwanza baada ya miaka tisa kwa timu nje ya Barcelona na Real Madrid kutwaa taji hilo, mara ya mwisho Valencia walikuwa mabingwa msimu wa 2003-2004.
Shujaa wa ubingwa; Diego Godin akishangilia boa lake lililoipa ubingwa Atletico
Barcelona walitangulia kupata bao dakika ya 34, mfungaji Alexis Sanchez aliyemalizia pasi ya Lionel Messi. Barcelona walipata bao hilo baada ya Atletico kupata pigo kwa wachezaji wake wawili tegemeo kuumia kwa mpigo ndani ya dakika 20 na kushindwa kuendelea na mchezo.
Alinza mfungaji wake tegemeo Diego Coasta dakika ya 16, ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Adrian kabla ya Arda Turan naye kuuminia dakika ya 20 na nafasi yake kucukuliwa na Raul Garcia.
Pamoja na hayo, timu ya Diego Simeone ilitulia na kumaliza dakika 45 wakiwa nyuma kwa bao hilo hilo 1-0, japokuwa mchezo ulitawaliwa na rafu nyingi kipindi hicho.
Kipindi cha pili, Atletico ambao wiki ijayo watacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Real Madrid walibadilika na kufanikiwa kusawazisha bao hilo.
Shukrani kwake Diego Roberto Godin Leal aliyefunga bao hilo muhimu dakika ya 49 akimalizia kwa kichwa kona ya Gabi.
Atletico imemaliza na pointi 90 baada ya mechi 38 wakati Barcelona imebaki nafasi ya pili kwa pointi zake 87 na Real ya tatu kwa pointi zake 86.
No comments:
Post a Comment