WATANZANIA nchini Italia, Jumamosi tarehe 26 Aprili 2014, walikutana mjini Roma kwenye ukumbi wa Ubalozi uliopo Viale Cortina d’Ampezzo 185, kusherehekea sikukuu ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Dkt. James A. Msekela.
Sherehe ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania Italia, Maofisa wa Ubalozi na familia zao, Maofisa wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Roma na familia zao pamoja na Watanzania waishio Italia.
Keki yetu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Bi. Mary Mtemahanji, mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzani Modena akiimba kwafuraha wakati wa kufungua champeign.
Bi. Zainab na Bw.Peter wakikata keki ya Muungano kwa pamoja.
Picha ya pamoja. Kushoto ni Katibu wa Jumuiya wa Watanzania Roma na pia Katibu wa Kamati ya Diaspora Italia Bw. Andrew Chole Mhella, katikati ni Bw. Peter na kulia ni Mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma Bw. Kondela Buhire.
Mheshimiwa Balozi Dkt. James Msekela akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italia Bw. Abdulrahmani A.Ali.
Kutoka kushoto ni Bw. Karim Msemo, Ofisa wa Ubalozi Roma; Bw. Peter na Bw. KondelaBuhire, mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma.
Mh. Balozi akisalimiana na Ndugu Andrew Chole Mhella, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma na pia ni Katibu wa Kamati ya Diaspora Italy.
Wakina mama wakifurahia picha ya pamoja.
Wadada wa Kitanzania wakipata picha ya ukumbusho. Tokea kushoto ni Bi.Lilian Luhende, Bi. Esther Mahella, Bi Riziki Habibu na Bi. Diana Olotu.
Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa Jumuiya za Watanzania Italia na Ofisa wa Ubalozi. Kutoka kushoto ni Katibu wa Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki wa Tanzania- Roma, Shemasi Romanus; Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italia Bw. Abdulrahmani Ali; Mwenyekiti wa Jumuiya wa Watanzania Roma, Bw. Erasmus Luhoyo, Ofisa wa Ubalozi, Bw. Karim Msemo na Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma, Bw. Andrew Mhella. Picha Zote zimepigwa na Mr. Karim Msemo wa Embassy of Tanzania in Italy
No comments:
Post a Comment