Askari
wa Usalama Barabarani akitoa elimu ya mabadiliko ya njia za katikati ya
Jiji la Dar es Salaam, kwa dereva wa gari dogo lenye namba za usajiri T
357 BZT, wakati likitaka kuelekea njia yenye alama inayozuia kupanda
kutokana na mabadiliko ya njia ambayo yameanza rasmi kutumika kuanzia
jana Aprili 28. Kwa sasa askari wa usalama Barabarani wameamua kusimama
kwenye njia panda zote kwa ajili ya kutoa elimu na maelekezo kwa
madereva wasioelewa mabadiliko hayo ama wasiosikia kuhusu mabadiliko
hayo kabla ya kuanza kuyakamata magari yanayokiuka muongozi wa njia
hizo.
Kutokana
na kwamba baadhi ya madereva bado hawajaelewa mabadiliko hayo, askari
hao wamekuwa wakisimama eneo husika na kuwasimamisha wakati wakitaka
kuelekea na kusha kuwapatia elimu na kisha kuwaruhu kuendelea hadi hapo
watakapositisha elimu hiyo na kuanza kuwakamata madereva wasiofuata
sheria na alama hizo. Hii ni barabara ya Karimjee ambayo kwa sasa
haiendi ukitokea Ocean Road.
Hii ni barabara ya Samora ambayo kwa sasa inapandisha ukitokea mzunguko wa Askari.....
Hii ni barabara ya mbele ya Maelezo na Jengo la IPS ambayo kwa sasa haielekei bali inapandisha usawa wa Mzunguko wa Askari....
No comments:
Post a Comment