Tuesday, April 1, 2014

BIBI WA MIAKA 68 AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KWA TUHUMA ZA KISHIRIKINA

“PRESS RELEASE” tarehe 01.04.2014. 
Bibi wa miaka 68 auawa na watu wasiofahamika kwa tuhuma za kishirikina.
mzee wa miaka 62 afariki dunia baada ya kuzidiwa na maji ya mto saza.
mtoto wa miaka 02 amekutwa amekufa maji baada ya kutumbukia ndani ya kisima.

katika tukio la kwanza:
Bibi wa miaka 68 aliyefahamika kwa jina la belta sanzia mkazi wa maweni ameuawa kwa kukatwa na kitu kinachodhaniwa kuwa shoka kichwani, mkono wa kulia na kutobolewa sehemu za ubavu wa kushoto na mtu/watu wasiofahamika.
Tukio hilo la kusitikisha limetokea majira ya usiku wa kuamkia tarehe 31.03.2014 huko katika kitongoji cha maweni, kijiji na kata ya mkwajuni, tarafa ya kwimba, wilaya ya chunya. inadaiwa kuwa chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina baada ya marehemu kutuhumiwa kuwaroga wanakijiji wenzake. 
marehemu alikuwa akiishi peke yake katika nyumba yake. juhudi zinaendelea kuwasaka waliohusika na tukio hilo. 
kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. msangi anatoa wito kwa jamii kuachana na imani potofu za kishirikina kwani zina madhara makubwa katika jamii. aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mtu/watu waliohusika na tukio hili azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Katika tukio la pili:
Mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la luchagula maenzeka (62) mkazi wa kitongoji cha kininga amekutwa amekufa maji ndani ya mto saza.
tukio hilo limetokea mnamo tarehe 31.03.2014 majira ya saa 09:30 asubuhi huko katika kitongoji cha kininga, kijiji na kata ya saza, tarafa ya kwimba, wilaya ya chunya. inadaiwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni marehemu kushindwa kuyamudu maji ya mto huo kutokana na ulevi hali iliyopelekea kusombwa na maji.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. msangi anatoa wito kwa jamii kuwa makini wanapovuka mito hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha kwani ni hatari. aidha anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kunywa pombe kupindukia kwani ni hatari si tu kwa afya zao bali hata kwa maisha yao.

Katika tukio la tatu:
Mtoto mdogo aliyefahamika kwa jina la julieta christian (02) mkazi wa saza amekutwa amekufa maji ndani ya kisima kilichopo jirani na nyumba wanayoishi.
tukio hilo limetokea mnamo tarehe 31.03.2014 majira ya saa 11:00 asubuhi katika kitongoji cha kati, kijiji na kata ya saza, tarafa ya kwimba, wilaya ya chunya. wakati tukio hilo linatokea marehemu alibaki peke yake nyumbani bila mwangalizi yeyote.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. msangi anatoa wito kwa wazazi/walezi kuweka uangalizi wa kutosha kwa watoto wao ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza. aidha anatoan wito kwa jamii kufunika visima vilivyowazi, kufukia madibwi na mashimo kwani ni hatari kwa watoto wadogo hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment