Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Serena Hotel Bw. Seraphin Lusala (katikati)akiangalia moja ya aina ya taa zinazotumia umeme mdogo wakati wa hafla ya Saa za Dunia (Earth Hour) jana jijini Dar es Salaam. Earth Hour ni harakati zinazofanyika kila mwaka duniani kote zikiwa na lengo mahususi la kutunza mazingira na nishati , katika hafla hiyo ambayo ufanyika kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi machi taa uzimwa kwa muda wa saa moja kuanznia saa 2:30 usiku hadi saa 3:300.kulia ni Afisa Mauzo wa kampuni ya Smart Sense Venu Sree na kushoto ni Mkurugenzi wa Smart Sense Bw. Kalpesh Babaria.
Mkurugenzi wa Smart Sense Bw. Kalpesh Babaria akitoa maelezo kuhusu taa aina ya LED ambazo zimebuniwa mahususi kupunguza matumizi makubwa ya nishati ya umeme na uharibifu wa mazingira,wakati wa hafla ijulikanayo kama Earth Hour ambayo lengo lake ni kuhifadhi na kutunza mazingira.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Bi. Neema Rose Singo akisoma maelekezo kuhusu taa za LED wakati wa hafla ya Earth Hour iliyofanyika Serena Hotel jana jijini Dar es Salaam, wanaofuatia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Dar es Salaam Serena Hotel Bw. Seraphin Lusala, Afisa Mauzo wa kampuni ya Smart Sense Venu Sree na Mkurugenzi wa Smart Sense Bw. Kalpesh Babaria.
Mkuu wa Masoko wa Exim Bank Tanzania Bw. Noel Tuga akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa kampuni ya Smart Sense Venu Sree kuhusu matumizi ya taa za kisasa aina ya LED ambazo zinatumia nishati kidogo.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Serena Hotel Bw. Seraphin Lusala (mwenye suti nyeusi) akifurahi pamoja na wageni na wafanyakazi wenzake baada ya kuadhimisha Saa ya Dunia (Earth Hour) jana jijini Dar es Salaam. Earth Hour ni harakati zinazofanyika kila mwaka duniani kote zikiwa na lengo mahususi la kutunza mazingira na nishati , katika hafla hiyo ambayo ufanyika kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi machi taa uzimwa kwa muda wa saa moja kuanznia saa 2:30 usiku hadi saa 3:30 usiku
Picha na Frank Shija
No comments:
Post a Comment