WITO umetolewa kwa wadau wa sheria kujitokeza na kuandika vitabu vitakavyowawezesha wananchi kuzifahamu sheria mbalimbali za ardhi ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa mpana juu ya umuliki wa ardhi yao.
Wito huo umetolewa na Prof. Anna Tibaijuka katika uzinduzi wa kitabu kinachozama kwa kina kuhusu sheria ya ardhi, Abdon Rwegasira kiitwacho ''LAND as a human right''
Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akiwahutubiwa wanazuoni na baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi wa kitabu hicho. |
Kubwa lililoongelewa katika uzinduzi huo na Prof. Anna Tibaijuka ni kuwa wadau wajitokeze kwa wingi kwani watanzania wengi wangependa kupata jumbe nyingi zilizo katika vitabu mbalimbali vinavyoelezea sheria ya Ardhi hasa ya Tanzania, lakini kwasababu vingi vimeandikwa kwa lugha isiyo ya kiswahili hivyo inakuwa ni changamoto kwao, lakini kutona na ujuio wa kitabu hicho, kitawapa wengi hamu ya kukisoma kwasababu kipo katika lugha wanayoielewa, licha ya kuwa lugha ya kiingereza bado ni changamoto.
No comments:
Post a Comment